Misa tarehe 18 Mei ya kuanza upapa rasmi wa Papa Leo XIV!
Vatican News
Dominika ijayo, tarehe 18 Mei 2025, majira ya saa 04:00 kamili asubuhi, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Papa Leo XIV ataongoza Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuanza utume rasimi utume wake wa kipapa, Papa wa Roma na Ulimwengu. Tukio hilo muhimu limetangazwa na Nyumba ya Kipapa,Ijumaa 9 Mei ambalo limechapisha ratiba ya Papa kwa mwezi wa Mei 2025.
Jumamosi tarehe 10 Mei, Baba Mtakatifu atakutana na Makardinali, wakati Dominika tarehe 11 Mei ataali sala ya Malkia wa Mbingu kutokea katikati ya Basilika ya Mtakatifu Petro. Mnamo Mei 12, atafanya mkutano na vyombo vya habari vya ulimwengu ambao vilikuwa vimekusanyika jijini Roma katika majuma ya hivi karibuni ili kuakisi matukio tangu ya kifo cha Papa Francisko hadi Conclave.
Tarehe 16 Mei 2025, mkutano umepangwa na Wanadiplomasia (na Wakuu wa Misheni), wakati huo huo Jumanne 20 Mei 2025, Papa Leo XIV atamiliki Basilika ya Kipapa ya Mtakatifu Paulo Nje ya Kuta. Siku itayofuata, atafanya katekesi yake ya kwanza ya Jumatano
Jumamosi tarehe 24 Mei 2025 mkutano mpya: wakati huu na Curia Romana na wafanyakazi wa mji wa Vatican. Dominika tarehe 25 Mei 2025 kutakuwa na sala ya Malkia wa Mbiungu na kisha tukio la kumiliki Mabasilika ya Kipapa ya Mtakatifu Yohane Laterano na Mtakatifu Maria Mkuu.
Ofisi ya vyombo vya Habari Vatican
Na Matteo Bruni, Msemaji mkuu wa Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican, akitaka kusisitiza katika hotuba ya kwanza ya Papa mpya Leo XIV, katika kituo cha habari muda mfupi baada ya kuchaguliwa kwake alisema Papa Leo XIV "alitumia maneno ya kwanza ya Yesu baada ya Pasaka, maneno ya amani, hasa ya kupokonya silaha”na alizungumza juu ya "mazungumzo".
Dk. Bruni alioneesha umuhimu wa jina lililochaguliwa na Papa mpya na kusema kuwa: "Ni kumbukumbu ya wazi" kwa mtangulizi wake Leo XIII, ambaye mnamo Mei 1891 alichapisha Waraka wa Rerum novarum, ambapo Mafundisho ya Kijamii ya kisasa ya Kanisa yanatoka humo. "Kwa wazi sio marejeo ya kawaida kwa wanaume na wanawake, kwa kazi zao, hata wakati wa Akili Mnemba alisisitiza," alisisitiza .
Dk Bruni pia aliongeza kusema jinsi ambavyo Papa mpya alivyozungumzia juu ya "mazungumzo", katika ulimwengu ambao mara nyingi huguswa na migogoro na mivutano. "Mungu anatupenda, anawapenda nyote na uovu hautashinda". Baraka hiyo ya Papa Leo XIV kiukweli pia alikumbusha baadhi ya maneno ya mwisho ya Papa Francisko aliyosema Dominika ya Pasaka.