Laudato si':Miaka 10 ya kilio cha Francisko kwa ulinzi wa nyumba ya pamoja
Hati ya "Canticle of the Creatures" yaani “Sifa kwa viumbe” ni jina lake ambalo lilichukuliwa kutoka katika wimbo wa Mtakatifu Francis wa Assisi, ambayo mara moja ikawa msingi wa Mafundisho ya Papa wa Argentina (Papa Francisko) na pia hatua ya kumbukumbu kwa mipango mingi kwa ajili ya asili na msukumo wa mipango ya kisiasa na kijamii. Hati hii inakusanya, katika mtazamo wa pamoja, tafakari mbalimbali za Mabaraza ya Maaskofu duniani kote na kuhitimisha kwa sala mbili, moja ya kidini na moja ya Kikristo, kwa ajili ya ulinzi wa kazi ya Uumbaji. Katika sura zake sita,za kujali kazi ya Uumbaji kunaunganishwa na wito wa haki kwa maskini, kujitolea kwa jamii, na mwaliko wa amani ndani yake. Wito muhimu sana wa Papa Francisko kwa ajili ya "uongofu wa kiikolojia",na kwa ajili ya "mabadiliko ya mwelekeo" ili mwanadamu achukue jukumu la kujitolea kwa kazi ya "utunzaji" wa nyumba yetu ya pamoja hii iliyotolewa na Bwana.
Ahadi inayotokana na imani ya Kikristo yenyewe.
"Kilio" cha Francisko miaka minane baadaye kilizinduliwa tena na Laudate Deum, Waraka mwingine wa kitume ambao uliandikwa na Papa Fransisko ambaye alibainisha kwamba, unakamilisha waraka wa 2015, ambamo Papa alibainisha majibu na hatua zisizotosheleza na kusisitiza tena dharura ya "hatua ya kuvunjika ambayo inakaribia.”
(Imandaliwa na Salvatore Cernuzio.Video imetengenezwa na Timu ya Wahariri ya mitandao ya kijamii Vatican).