Ujumbe wa uongo kwa rais wa Burkina Faso unaohusisha Papa
Vatican News
"Kwa Mheshimiwa Rais Ibrahim Traoré, Rais wa taifa huru la Burkina Faso, mwana wa ardhi ya Afrika, mlinzi wa watu wake, neema na amani ziongezwe kwako kupitia hekima, ujasiri na ukweli ...". Hivyo ndivyo unaanza ujumbe wa uongo kwa lugha ya Kiingereza kuhusishwa na Papa ambao umeundwa na Akili Nunde(AI). Hotuba ya takriban dakika 36, ??kwa Kiingereza, iliyopakiwa kwenye YouTube na akaunti ya "Pan African dreams" na kuundwa kwa kutumia picha za Mkutano wa Papa Leo XIV na waandishi wa habari siku ya Jumatatu tarehe 12 Mei 2025. Ilitumiwa "Morping", yaani, mbinu inayobadilisha picha kwa kufanya harakati ya midomo iendane na maneno yaliyopotoshwa na akili Nunde(AI). Video hiyo ya uwongo inaitwa: "Papa Leo XIV anamjibu Kapteni Ibrahim Traoré - Ujumbe wa Ukweli, Haki & Upatanisho."
Wale wanaoitazama wanaongozwa kuamini kwamba Papa mpya alihutubia hotuba nzima ya Mkutano na Rais wa Burkina Faso, Ibrahim Traoré akijibu mojawapo ya barua zake, na katika video hiyo Papa Leo ametolewa akisema: "Nimesoma maneno yako sio mara moja, lakini mara nyingi, na kila usomaji umekuwa wa kina zaidi kuliko ule uliopita, kwa sababu kwa sauti yako sijasikia tu hasira ya rais, lakini kilio cha haki cha bara lililojeruhiwa kwa muda mrefu na ncha mbili za kutelekezwa na unyonyaji."
Video hiyo ni sehemu ya safu ya jumbe za kughushi ambazo pia zilijadiliwa mnam Mei 15 iliyopita hata na , na ilizinduliwa upya katika toleo fupi zaidi na yenye ubora wa chini wa picha pia na akaunti ya YouTube "Nou se Legliz." Ni dhahiri kwamba picha ya Papa inarudiwa na Leo kila wakati anageuza karatasi zile zile kwa muda wote wa ujumbe.
Inafaa kukumbuka, kutokana na kusambazwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii ya maandishi yanayohusishwa na Papa mpya bila kuashiria chanzo, cha hotuba zote, lazima kila wakati uingiliaji kati, wa maandiko ya Papa Leo XIV ambapo unaweza kushauriwa kwa ukamilifu kupitia kwenye tovuti: . Ingawa habari kuhusu shughuli zake na jumbe zake za video zinaweza kushauriwa kwa wakati halisi kwenye tovuti ya lango lake: Vatican News, vaticannews.va, na inapatikana katika lugha mbalimbali na pia kwenye tovuti ya gazeti la kila siku la Vatican la: la Osservatore Romano, . Hapa utapata habari za ukweli kuliko kusikiliza za uongo!