杏MAP导航

Tafuta

2025.04.30 Gari la Papa Francisko ni zawadi kwa watoto wa Gaza. 2025.04.30 Gari la Papa Francisko ni zawadi kwa watoto wa Gaza.  (Caritas )

Gari la Papa la amani:Zawadi ya mwisho ya Papa Francisko kwa Gaza!

Papa ameomba“杏MAP导航mobile,”gari lake ligeuzwe kuwa zahanati inayotembea ya watoto wa Ukanda huo.Caritas Yerusalem:"Sio gari tu,bali ukaribu wa Papa kwa walio hatarini zaidi."

Vatican News

Urithi wa amani wa Papa Francisko unaendelea kung'aa katika ulimwengu wetu uliojaa migogoro. Ukaribu huo uliooneshwa kwa walio hatarini zaidi wakati wa utume wake unapata mwangwi hata baada ya kifo chake na mshangao huu kwa dunia nzima kutokana na “杏MAP导航mobile” yaani gari lake, lile lile alilotoka nalo mara kwa mara kuwasalimia na kuwakaribia mamilioni ya waamini duniani kote, na ambalo sasa linageuzwa kuwa kitengo cha afya kinachotembea kwa ajili ya watoto wa Gaza. Ilikuwa ni matakwa yake ya mwisho kwa watu alioonesha mshikamano mkubwa katika kipindi chake chote cha Upapa, hasa katika miaka ya hivi karibuni tangu kuanza kwa vita vya wao kwa wao. Na katika miezi yake ya mwisho, Papa alikabidhi mpango huo kwa Caritas Yerusalem, akitaka kujibu mzozo mbaya wa kibinadamu katika Ukanda huo, ambapo karibu watoto milioni sasa wameyakimbia makazi yao

Gari la Papa Francisko kwa ajili ya zahanati inayotembea huko Gaza
Gari la Papa Francisko kwa ajili ya zahanati inayotembea huko Gaza   (Caritas)

Huku kukiwa na vita mbaya, kuporomoka kwa miundombinu, mfumo wa afya uliodumaa na ukosefu wa elimu, watoto ndiyo wa kwanza kulipa gharama hiyo, huku njaa, maambukizi na hali nyingine mbaya za kiafya zikiweka maisha yao hatarini. Papa Francisko aliwahi kusema kwamba "watoto sio idadi ya kuhesabu. Ni nyuso. Majina. Historia. Na kila mmoja wao ni mtakatifu,” na kwa zawadi hii ya hivi karibuni, maneno yake yameendelea kuwa vitendo hata baada ya kifo. Gari la Papa ambalo  tayari limepewa jina la "The Vehicle of Hope" “Gari la Matumaini- limepambwa kwa vifaa vya kutambua, kuchunguza na kutibu hali, ikiwa ni pamoja na vipimo vya haraka vya maambukizi, zana za uchunguzi, chanjo, vifaa vyote vingine vya kuokoa maisha.

Gari la Papa alilotembea nalo kwa ajili ya Gaza
Gari la Papa alilotembea nalo kwa ajili ya Gaza

Pia itakuwa na vifaa vya madaktari na wahudumu wa afya na - mara tu ufikiaji wa kibinadamu katika Ukanda huo utakaporejeshwa - utawafikia watoto katika pembe za kipekee za Gaza. Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Peter Brune, katibu mkuu wa Caritas Sweden, ambayo pia inaendeleza mpango huo kupitia michango kutoka kwa waamini wakati wa Majilio, aliandika kwamba "kwa gari hilo, tutaweza kuwafikia watoto ambao leo hawawezi kupata huduma za afya, waliojeruhiwa na watoto wenye utapiamlo." "Huu ni uingiliaji madhubuti na wa kuokoa maisha wakati mfumo wa afya huko Gaza karibu kuporomoka kabisa," aliongeza. Yerusalem, ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikihudumia jamii za Gaza katika hali ngumu, inaongoza juhudi mahalia. Pamoja na wafanyakazi zaidi ya mia moja wanaohusika katika kutoa huduma za afya, shirika sasa linajenga juu ya urithi wa Papa wa huruma na nguvu, na kuleta baraka zake za mwisho kwa watu wa Gaza. "Gari hili linawakilisha upendo, utunzaji na ukaribu wa Utakatifu Wake kwa walio hatarini zaidi, ambayo ameelezea wakati wote wa shida," Anton Asfar, katibu mkuu wa Caritas Yerusalem. Gari linaonekana kuwa imechukuliwa kwa uangalifu kwa mahitaji ya wale wanaohitaji zaidi. Lakini “si gari tu, bali ni ujumbe ambao ulimwengu haujawasahau watoto wa Gaza." Na pia ni mwaliko  kwamba ulimwengu wote uwakumbuke pia.

Papamobile:gari la Papa nchini Gaza
05 Mei 2025, 10:21