Cascia:Siku kuu ya Mtakatifu Rita kwa baraka na salamu za Papa Leo XIV
Na Tiziana Campisi na Angella Rwezaula Vatican.
Salamu na sala kwa waamini na mahujaji ambao tarehe 22 Mei 2025 huko Cascia walifanya kumbukumbu ya kiliturujia ya Mtakatifu Rita. Baba Mtakatifu Leo XIV alimkabidhi Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Agostino, Padre Alejandro Moral, aliyeshiriki misa hiyo, katika Madhabahi ya Kipapa ya mji wa Umbria iliyoongozwa na Kardinali Bardo Reina, Makamu wa Papa, Jimbo la Roma. Mwishoni mwa liturujia, Padre huyo aliwaeleza wale waliokuwapo maneno ya Papa Leo XIV kwamba: “walikutana naye Jumatatu ya Juma hili (Mei 19)akamuuliza kama alikuwa anakwenda Cascia na hivyo akajibu ndiyo na kumtuma salamu yake na maombi yake.
Maelfu ya waridi na sala
Mamia elfu ya watu walikuwepo kwenye Misa hiyo, wakiwa wameshika mawaridi mikononi mwao, maua ambayo ni ishara ya Mtakatifu Rita, yaliyounganishwa na muujiza wa maua ya ajabu, katikati ya kipindi cha baridi sana na theruji, mahali alipozaliwa Roccaporena, kilomita tano hivi kutoka Cascia; na pia kukumbusha miiba yake na shida alizopata, pamoja na manukato yake. Na ilikuwa hasa kwa misukosuko ya Rita kwamba Kardinali Reina wakati wa mahubiri yake alirejea historia ya maisha yake huku, akikumbuka shida za maisha yake kuanzia: ndoa yake ngumu, mume wake aliyeuawa, watoto wake wawili waliokufa na kisha maisha ya kitawa ambayo mwanzoni hakukubaliwa na hatimaye kukumbatiwa, lakini kwa mateso mengi na mateso ambayo yalifuatana naye, na mwiba wa maisha yake, hadi mwisho wa maisha yake." Kardinali Reina alisema “angeweza kutumia maovu mengine na pengine pia angepata kibali cha wengine lakini alipendelea njia tofauti, hasa ile njia ya Injili, ya kupendelea kusamehe.”
Zawadi ya Amani
“Tukitazama leo hii, wakati uliowekwa na hali ya kutisha ya vurugu, ghasia zilizoenea na matukio ya vita ambayo yanatutia wasiwasi kweli, na vita vya tatu vya dunia vilivyomegeka vipande vipande, kama Papa Francisko alivyopendelea kusema”, Kardinali alisisitiza maneno ya kwanza ya Baba Mtakatifu Leo XIV, ambaye, wakati wa kujitokeza katikati ya dirisha la Baraka ya kwanza ya URB et ORBI,mara baada ya zawadi yake ya amani, alisema: "Leo tuna wasiwasi sana juu ya kile kinachotokea ulimwenguni kote, kuhusu vita vingi ambavyo kiukweli havikomi, kupungua, kuna ongezeko kubwa la jeuri," na akasisitiza kwamba "uovu hauwezi kushindwa kwa uovu zaidi" na mwaliko wa Papa wa ulikuwa wa “kuondoa silaha za lugha.” Kwa kususitiza zaidi Papa Leo XIV alisema:"Tunahitaji kupokonya hisia, ili kunyang'anya silaha mioyoni mwetu. Tunahitaji kufikiria njia nyingine za kujenga mahusiano ambayo ni ya kibinadamu kabla ya kuwa ya Kikristo."
Kutoka kwa Cascia kuna harufu ya udugu ambayo inaweza kung'aa
Kwa upande wa Kardinali Reina akidadavua Injili iliyosomwa ya siku pia alisema “kukaa ndani ya Kristo, katika upendo wake, kama tawi la mzabibu, ndivyo uovu unavyoweza kushindwa, kwa sababu “Yeyote anayekaa ndani ya Mungu hawezi kutokuwa mwaminifu. Yeyote anayekaa ndani ya Mungu hawezi kudharau wanyonge, yatima, mjane, mgeni, kwa sababu upande wa Mungu daima kuna mema, " alisisitiza, huku akifafanua kwamba "Siri ya Rita ilikuwa hii: alibaki katika Mungu, daima. Mtakatifu Rita alikuwa mwanamke aliyejawa na furaha, hata katika shida. Kwa njia hiyo alihitimisha Kardinali kwa matumaini kwamba kutoka Cascia "harufu ya utakatifu, udugu, wema inaweza kung'aa.”