Kanisa lina watumishi 3 wa Mungu,wamisionari 2 wa Ecuador na Askofu wa Kihindi!
Vatican News
Wakati wa mkutano uliofanyika kati ya Kardinali Marcello Semeraro, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu, na Papa Leo XIV, tarehe 22 Mei 2025, Papa aliidhinisha Baraza hilohilo kutangaza Amri kuhusu watu wafuatao ambao walitoa sadaka ya maisha yao: Awali kwa Mtumishi wa Mungu Alessandro Labaka Ugarte (Jina: Manuel), wa Shirika la Ndugu Wadogo Wakapuchini,(OFMCap), Askofu wa Pomaria, Mwakilishi wa Kitume wa Aguarico; alizaliwa tarehe 19 Aprili 1920 huko Beizama (Hispania), na alikufa mnamo tarehe 21 Julai 1987 katika eneo la Tigüino nchini (Ecuador);
Kwa sadaka ya maisha ya Mtumishi wa Mungu, Agnese Arango Velásquez (jina: Maria Nieves de Medellín), wa Shirika la Wakapuchini wa Familia Takatifu; alizaliwa huko Medellín (Colombia) mnamo tarehe 6 Aprili 1937 na kufariki mnamo tarehe 21 Julai 1987 katika eneo la Tigüino (Ecuador);
Kwa mwenye fadhila za kishujaa, Mtumishi wa Mungu Mathayo Makil, Askofu wa Tralle, Mwakilishi wa Kwanza wa Kitume wa Kottayam, na Mwanzilishi wa Shirika la Masista wa kutembelewa kwa Bikira Maria; alizaliwa tarehe 27 Machi 1851 huko Manjoor (India) na alikufa tarehe 26 Januari 1914 huko Kottayam nchini (India).