杏MAP导航

Tafuta

Castel Gandolfo,hisia kwa mshangao wa kuwasili kwa Papa

Tiziana Campisi - Castel Gandolfo

Habari zilienea karibu saa 5.00 asubuhi sikisema: "Papa yuko Castel Gandolfo!!!." Na zilienea haraka kati ya watu wa Castel Gandolfo, wakazi na wenye maduka, ambao ndani ya dakika chache walikimbilia kwenye uwanja wa mji, Uwanja wa uhuru, mbele ya Jumba la Kitume. Maneno ya mdomo ni ya haraka na wenye maduka waliacha haraka mikahawa yao, maduka na maduka ya zawadi na kukimbia hadi chemchemi, katikati ya Uwanja. Kulikuwa na furaha na udadisi, kila mtu alitarajia kuona Papa Leo XIV na walikaa kwa muda wa saa moja kusubiri.

Jumba la Kipapa la Castel Gandolfo
Jumba la Kipapa la Castel Gandolfo
Castel Gandolfo
Castel Gandolfo

Ziara ya kibinafsi na kituo cha Borgo Laudato si'

Ziara ya Papa ilikuwa ni ya faragha, ambayo haikujumuisha matukio ya umma. Kusimama katika bustani hiyo ya Borgo Laudato si', ni mpango wa kuhamasisha ikolojia fungamani  ulioanza miaka miwili iliyopita, kwa amri ya Papa Francisko, kisha kwenda  kwenye Jumba la kitume. Kwa upande wa Davide alisimulia nyakati zenye shughuli nyingi za mbio za kwenda uwanjani na dakika alizotumia kupiga gumzo na wauza maduka na wakazi huku wakisubiri angalau kusalimiana na Papa kutoka mbali. Naoual, Mwislamu, pia alikimbilia huko. Aldo, anayeishi katika eneo dogo la Corso della Repubblica lililoezekwa kwa mawe ya kale, alikuwa ametoka tu nyumbani kwake na alinaswa na mazingira ya sherehe ambayo yalilipuka ghafula. Kila mtu alifurahishwa na uwepo wa Papa Prevost mahali ambapo Mapapa wengi walichagua kutumia wakati wa likizo za kiangazi.

Castel Gandolfo
Castel Gandolfo
Castel Gandolfo
Castel Gandolfo

Uhusiano wa mapadre na Mapapa

Mgahawa unakumbusha kumbukumbu, nyakati ambazo Papa Paulo VI alikaa huko Castel Gandolfo na alikumbuka kwamba leo ni kumbukumbu yake(tarehe 28 Mei). Alifafanua kwamba washiriki wa castel wana uhusiano maalum na Papa na ni matumaini kwamba Papa Leo XIV atachagua kukaa siku chache katika miezi ijayo. Katika bar moja, mvulana kwenye kaunta hakuweza kuficha shauku yake kwa "mshangao wa Papa", angependa kusalimiana na Papa, lakini alifurahi vile vile kuhusu ziara hiyo isiyotarajiwa. Paroko wa Parokia ya Kipapa ya Mtakatifu Tommaso wa Villanova, Tadeusz Rozmus, alitafsiri hisia za watu wa Kanisa, wote wakiwa na msisimko wa uwepo wa Papa. “Hii, kwao, itabaki kuwa siku ya kukumbuka.  Bwana harusi anayesubiri nusu yake bora aolewe katika parokia ya kipapa anafurahi sana, na anazungumza juu ya "baraka" akimaanisha kukaa kwa muda mfupi kwa Papa Leo XIV siku ya harusi yake.” Papa aliondoka Castel Gandolfo mapema mchana, huku kukiwa na nderemo na vifijo kutoka kwa mamia ya watu waliokusanyika kando ya barabara. Watoto wengi wakiwa na wazazi wao walitaka kumsalimia. Usalama wa umma ulijaribu kuzuia umati. Na Papa  Leo XIV, kwenye gari dogo, kwenye kiti cha mbele, alitabasamu na kurudisha salamu kwa kuinamia nje ya dirisha. Kisha akaondoka kurudi mjini Vatican.

30 Mei 2025, 14:39