Asanteni!Yalikuwa ni maneno ya kwanza ya Papa Leo XIV katika kuta za Vatican!
Na Isabella Piro na Angella Rwezaula – Vatican.
"Asante!" Kwa upendo na shukrani, Papa Leo XIV alitoa shukrani hizo kwa wakazi wa Jumba la Nyumba Takatifu za ofisi (Sant'Uffizio) jana jioni, Alhamisi tarehe 8 Mei 2025. Ilikuwa ni saa chache baada ya kuchaguliwa kwa Kiti cha Kharifa wa mtume Petro, katika safari yake ya kwanza kutoka kwenye Kuta za Vatican Papa mpya alikwenda mahali ambapo alikuwa anaishi kwa miezi miwili iliyopita - au tuseme, majuma saba, kama yeye mwenyewe alivyobainisha, ambapo bamba rahisi kwenye mlango wa kuingilia bado linasomeka "Robert Card. Prevost."
Makofi na kupeana mikono
Akishangiliwa na makofi yakushutukiza, Papa Prevost akiwa kwenye gari hadi ua wa Jumba la Ofisi takatifu. Vazi lake jeupe likiwa linaonekana nje kwenye giza la jioni, alisalimia kila mmoja wa wale waliohudhuria kwa kupeana mkono, pia akibadilishana maneno machache kwa lugha ya kihispania na baadhi ya waamini kutoka Mexico na Venezuela. Pia alikuwepo mtawa wa Xaverian Mfaransa, Nathalie Becquart, Katibu Msadizi wa Sinodi ya Maaskofu, ambaye katika chapisho la X - aliandika: "Nina furaha kukutana na kumpongeza Papa wetu mpya wa Sinodi ambaye anarudi kwenye Ikulu yetu ambako aliishi!"
Lazima nijaribu saini mpya
Kisha, msichana mdogo anayeitwa Michela alimkaribia kwa woga na kumwomba abariki Biblia na kutia saini. Papa Leo XIV alikubali ombi la mara mbili kwa furaha na, kwa kugusa kwa ucheshi, aliongeza: "Bado ninapaswa kupima saini, kwani ya zamani haihitajiki tena!" Kisha, ili kuwa na uhakika wa kutofanya makosa, alimwomba msichana mdogo kuandika jina lake na hatimaye, akiweka tarehe karibu na saini, aliongeza kwa utani: "Ni siku gani leo hii? Mei 8?".
Selfi na waliokuwapo
Papa Prevost kisha aliwabariki waamini, akimalizia maneno yake kwa: "Hongera! Asante!". Hatimaye, hakukataa ombi la baadhi ya waliokuwepo waliopendekeza kupiga selfi. Hapo awali, mara tu baada ya baraka ya kwanza ya Urbi et Orbi kutolewa karibu saa 1:30 jioni kutoka katikati ya Kanisa kuu la Vatican, Papa wa 267 pia alikuwa amewasalimia waamini mbali mbali waliokuwa wakimsubiri mbele ya Nyumba ya Mtakatifu Marta na waliomkaribisha kwa maneno ya "Uishi muda mrefu Papa!." Maneno ya furaha ambayo mrithi wa Petro aliitikia kwa ishara ya salamu, kabla ya kurudi mahali alipokuwa akiishi wakati wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi(Conclave.)