Papa anaendelea kupata nafuu kati ya kupumzika na kazi.Mkutano na Kard.Parolin
Vatican News
Hali ni ya kawaida, isipokuwa ile ya mshangao wa Dominika iliyopita, wakati alionekana kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, kwa mshangao wa kila mtu, wakati wa Misa ya Jubilei ya Wagonjwa na ya Ulimwengu wa kiafya ambayo bado imeenea ya siku za Papa Francisko, na ambaye kwa "roho nzuri" ameendeleza kupata nafuu kwa zaidi ya majuma mawili sasa katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican. Kwa hiyo “kupumzika, sala, kukonselebrate kila asubuhi katika Kikanisa cha ghorofa ya pili na kisha kupiga simu chache, kwa mtiririko wa kawaida wa simu za video kwa Parokia ya Gaza, kufanya kazi na washirika wake wa Mabaraza ya Kipapa huku akibadilishana nao simu na nyaraka. Na hatimaye, kuanza kwa taratibu kwa mikutano, ambapo Jumatatu tarehe 7 Aprili 2025 , Papa alimpokea Katibu wa Vatican Kardinali, Pietro Parolin, huko Mtakatifu Marta. Huu ndio ulikuwa mkutano wa kipekee kuwa nao, tangu aliporuhusiwa kutoka Hospitali ya Gemelli.
Hayo ndiyo yaliyoelezwa katika Ofisi ya Waandishi wa Habari Vatican, Jumanne tarehe 8 Aprili 2025, kwa kutoa sasisho kadhaa juu ya hali ya Afya ya Baba Mtakatifu Francisko pia juu ya shughuli zake katika siku za hivi karibuni na siku zijazo.
Maboresho kidogo
Kuhusu afya yake, hali ya Papa Francisko ni shwari huku kukiwa na maboresho kidogo katika vipengele vyake muhimu vya mazoezi ya kimwili, kupumua na sauti. Hili lilidhihirika Dominika iliyopita (Aprili 6) wakati waamini 20,000 waliokuwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro lakini pia waliokuwa wakifuatilia kwenye mitandao ya kijamii mbashara, waliweza kumuona Papa na kusikiliza salamu zake fupi akisema: “Dominika njema ninyi nyote na asanteni sana.”
Kuhusu “maambukizi ya mapafu bado yapo lakini yanapungua kidogo kidogo." Katika kuendelea kupata nafuu na kulindwa kwa umakini ambao haujawahi kukatishwa, na Papa daima anafuatilia maagizo aliyopewa na madaktari wanaomsaidia. Hata uchaguzi wa kwenda kwenye Uwanja, siku mbili zilizopita kwa hakika ulifanywa katika muktadha wa mapendekezo ya madaktari, lakini hakika ilitokea kutoka katika shauku ya Papa ya kushiriki katika wakati huu wa ukaribu na mahujaji wagonjwa."
Oksijeni na matibabu
Katika muktadha huo wa maendeleo madogo, ambayo tayari yameonekana katika siku za kwanza za kupona, Papa Francisko anatumia kila siku ya oksijeni: mtiririko wa juu wa oksijeni ni wakati wa saa za usiku tu kama unahitajika. Hali halisi kwa ujumla inabaki shwari kwa mtazamo wa vipimo vya kliniki. Hakuna taarifa juu ya vipimo vyovyote au X-ray zilizofanywa kwa Papa katika majuma haya. Ofisi y Waandishi wa Habari imethibitisha hata hivyo, kuendelea kwa tiba ya dawa na mazoezi ya viungo na kupumua.
Kazi inaendelea
Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican inasisitiza zaidi, ikieleza kwamba: “ Papa anendelea na kazi na kuwasiliana na wakuu wa Mabaraza ya Kipapa mbali mbali na anapokea nyaraka na katika siku za hivi karibuni ameanza tena baadhi ya mikutano." Mikutano ya hadhara haijaatazamiwa tena na haionekani kwamba itaanza tena hivi karibuni: na Katekesi ya tarehe 9 Aprili haitakuwapo lakini, kama ilivykuwa katika majuma ya hivi karibuni, maandishi yatatolewa.
Hakuna utabiri wa ibada za Pasaka
Kuhusina na ibada za Pasaka, siku chache kabla ya kuanza, bado hakuna maelekezo juu ya maadhimisho ya Juma Kuu Takatifu na juu ya uwezekano wa uwepo wa Papa katika ibada za (Triduum) yaani Siku Tatu Kuu za Juma Kuu Takatifu, na kwamba: "zitatathminiwa dakika baada ya muda." Inawezekana, hata hivyo, kwamba baadhi ya maelezo yatawasilishwa katika siku chache zijazo.