Rais Mattarella kwa Papa:Pasaka inaweza kuleta faraja kwa wale wanaoishi katika migogoro!
Vatican News
Rais wa Jamhuri ya Italia, Bwana Sergio Mattarella, Dominika tarehe 20 Aprili 2025 alituma matashi mema ya dhati ya Pasaka njema na takatifu kwa Papa Francisko. Katika ujumbe huo Mkuu wa Nchi ya Italia alikumbusha kwamba: "mwaka huu Makanisa yote ya Kikristo yameadhimisha sikukuu muhimu zaidi ya mwaka wa kiliturujia katika tarehe hiyo hiyo. Kwa njia hiyo muktadha huo wenye ishara kubwa, unatuhimiza kutafuta mazungumzo na umoja".
Kumbukizi ya somo wa Papa Mtakatifu George 23 Aprili
Kisha alionesha matumaini kwamba, "kwa kuhusishwa na Jubilei ya Matumaini, sherehe ya Pasaka italeta faraja kwa jamii ambazo katika mabara tofauti mara nyingi wanapata hali za migogoro au hatari." Ukumbusho wa Ufufuko ni matashi ya Rais Mattarella ya "kuwatia moyo hata wale wenye imani tofauti na Ukristo na wasioamini, ili kutafuta faida ya wote kushikanisha maadili ya haki na usawa, ambayo ni muhimu kwa kuishi pamoja kwa amani na ustawi wa watu.” Hatimaye, kwa niaba ya watu wa Italia, Rais alimtuma Papa heri ya Pasaka pia kwa sikukuu inayokaribia ya Mtakatifu George ifanyiakyo kila tarehe 23 Aprili ambayo ni siku ya jina la Papa kwa ubatizo: Jorge Mario Bergoglio.