Papa:Upendo wa Mungu ni wa bure badilika uwe na uhusiano na Mungu!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kama kawaida ya kila Jumatano, Baba Mtakatifu pamoja na kuendelea kupata nafuu katika Nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican, hakukosa kuandaa kama mwendelezo wa “Mzunguko wa Katekesi ya Jubilei ya 2025 kuhusu Yesu Kristo, Tumaini letu: Maisha ya Yesu. Mikutano mingine. Jumatano tarehe 9 Aprili 2025, amejikita na sehemu ya IV ya kijana tajiri. Yesu alimkazia macho (Mk 10,21). Injili iliyoongoza katekesi hii iliyochapishwa na Ofisi ya Vyombo vya habari, imetoka Mk 10, 17-22), kuhusiana na kijana tajiri aliyeomba afanye nini ili kuurithi Ufalme wa Mbingu. Baba Mtakatifu kwa njia hiyo anabainisha kuwa “leo tutafakari juu ya mkutano kati ya mingine ya Yesu iliyosimuliwa na Injili. Kwa mara hii, lakini mtu aliyekutana naye hajulikani jina. Mwinjili Marko anawakilishwa kwa urahisi kama “mtu mmoja”(Mk 10,17. Ni mtu ambaye tangu akiwa kijana alikuwa ameshika amri, lakini licha ya hayo alikosa maana kamili ya maisha. Yuko anatafuta. Labda ni mmoja aliyekuwa hajaamua kwa kina, licha ya ujuu juu wa mtu aliye na shughuli. Mbali na hayo kiukweli, mambo ambayo tunafanya, ya kijisadaka, au mafanikio, kile kinachohesabika kweli, ili uweze kuwa na furaha, ni kile tulicho nacho rohoni. Ikiwa meli itaondoa nanga na kuacha bandari ili kwenda kuelekea bahari iliyo wazi, inawezakana kuwa meli ya kushangaza, kwa kuwa na wafanyakazi wa kipekee, lakini ikiwa hawatavuta kamba na nanga zinazoishikilia, haitaweza kuondoka kamwe. Mtu huyu alitengeneza meli ya kifahari, lakini alibaki bandarini!
Kusahau neno la kutoa bure
Hata alipokuwa akitoka kwenda njiani, mtu mmoja akaja mbio, akampigia magoti, akamwuliza, Mwalimu mwema, nifanye nini nipate kuurithi uzima wa milele? (Mk 10,17). Hapa tunapata maneno: Nifanye nini ili nipate uzima wa milele.” Hii ni kwa sababu ya kushika amri kwake hakukumpatia furaha na usalama wa kuokoa, na ndipo almwelekea Mwalimu Yesu. Kile kinachoshangaza, ni kwamba mtu huyo hajuhi msamiati wa neno la “kutoa bure.” Kila kitu kilionekana kuwa kinafaa. Kila kitu ni wajibu. Baba Mtakatifu Francisko amekazia kusema kuwa maisha ya milele kwake yeye ni urithi, kitu ambacho unakipata moja kwa moja, kwa njia ya ushikiliaji makini wa kazi. Lakini maisha ya kuishi hivi kwa hakika haya ya mema, ni nafasi ipi inawezekana kuwa nayo ya upendo?Kama kawaida ya Yesu daima anakwenda zaidi ya ujuu juu. Ikiwa kwa upande mmoja mwanaume huyo anamwekea mbele wasifu wake, Yesu anakwenda zaidi na kutazama ndani. Neno ambalo atumia Marko ni la maana sana, akisema “alimtazama ndani (Mk 10,21). Hii ni kwa sababu Yesu hasa anatazama ndani ya kila mmoja wetu, na anatupenda kweli jinsi tulivyo. Ni kitu gani kiukweli aliona ndani ya mtu huyo? Yesu anaona nini wakati anatazama ndani mwetu na anatupenda, licha ya kutojali kwetu na dhambi zetu? Anaona udhaifu wetu, lakini pia hata shauku ya kuwa wapendwa jinsi tulivyo.
Yesu alimtazama kwa ndani na kumpenda
Kwa kumtazama ndani, Injili inabainisha, “alimpenda (Mk 17,21.) Yesu anapenda mtu huyo kabla hata ya kumpa mwaliko wa kumfuata. Anampenda jinsi alivyo. Upendo wa Yesu ni wa bure: kwa hakika kinyume cha mantiki ya kustahili ambayo ilikuwa imemzunguka mtu huyo. Tunafurahi kweli, tunapotambua ya kuwa tu wapendwa jinsi tulivyo, bure na kwa neema. Hii ni sawa sawa, hata na mahusiano kati yetu kwa sababu “ikiwa tutajaribu kununua upendo au kuomba kwa upendo, mahusiano hayo hayatatufanya tuwe na furaha.” Pendekezo la Yesu, analofanya kwa mtu huyo ni kubadili namna yake ya kuishi na mahusiano yake na Mungu. Yesu kiukweli anajua kwamba ndani yake, kama ilivyo kwetu sisi, kuna ukosefu fulani. Ni shauku ambayo tunaibeba ndani ya mioyo ya kuwa tulipendwa. Kuna jeraha ambalo linatuhusu kama watu kibinadamu, jeraha kwa njia ambayo upendo unaweza kupita. Na ili kutuliza ukosefu huu hatuhitaji kujionesha, kutambuliwa, kupendwa zaidi, kufikiriwa zaidi, kinyume chake inahitajika kuuza kila kitu kinachotuelemea, ili tuweze kuwa huru katika mioyo yetu. Hakuna maana ya kuendelea kuchukua kwa ajili yetu wenyewe, lakini badala yake kutoa kwa maskini na kufanya kupatikana na kushirikisha wengine.
Huzuni ni ishara ambayo waweza kuondoa
Hatimaye Yesu anamwalika mtu huyo hasibaki peke yake. Anamwalika amfuate, abaki ndani ya uhusiano wa kuishi kwa mahusiano. Ni kwa njia hiyo tu, kiukweli, itawezekana kutambuliwa kwa jina. Tunaweza kusikililiza jina letu tu ndani ya uhusiano, mahali ambamo kuna mtu anayetuita. Ikiwa tutabaki peke yetu, hatutaweza kusikia tunaitwa jina letu, na tataendelea kubaki (mtu “fulani” bila jina. Labda leo hii hasa kwa sababu tunaishi katika mantiki ya utamaduni wa kujitosheleza na ubinafsi, tunajigundua kutokuwa na furaha zaidi, kwa sababu hatuhisi kutamkwa tena jina letu na mtu anayetupenda bure. Na Mtu huyo hakukubali mwaliko wa Yesu na alibaki peke yake, kwa sababu kamba za maisha yake zilikuwa zimekaza katika bandari. Huzuni ni ishara ambayo hakuweza kuondokana nayo. Kristo, kwa upande mwingine, huona zaidi ya sura na mali ambazo tunafikiri in utajiri kumbe ni mizigo tu ambayo inatuzuia. Ni matumaini kwamba mtu huyo, kama ilivyo kwetu sisi, mapema au baadaye anaweza kubadilika na kuamua kutweka hadi kilindini. Baba Mtakatifu Francisko alihitimisha kwamba “tuwakabidhi katika Moyo wa Yesu watu wenye huzuni, na wasioamua, ili waweze kuhisi mtazamo wa upendo wa Bwana ambaye anakuwa na huruma kwa kutazama kwa huruma ndani ya mioyoni mwetu.