Papa kwa wanahija mbele ya matatizo ya ulimwengu tudumishe maombi!
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Francisko amewatumia ujumbe wanahija wa majimbo ya Grosseto na Pitigliano-Sovana-Orbetello, tarehe 9 Aprili 2025 katika fursa ya hija yao ya Matumaini mjini Vatican. Katika ujumbe huo, Baba Mtakatifu amewakaribisha na kumsalimia Askofu wao mpya, Mwashamu Askofu Bernardino Giordano, pamoja na kila mmoja wao, wasafiri wa kwenda Roma kwa ajili ya Jubilei. Papa amesema: “Njia ya kupitia Mlango Mtakatifu ipyaishe kila mtu katika imani, ili tuweze kutembea pamoja, mchungaji na zizi lake.”
Tudumu katika maombi na kuwa chumvi ya dunia
Papa Francisko ameelekeza mawazo yake hasa “kwa wale ambao ni wagonjwa na wazee miongoni mwa mengine kwamba “tuishi wakati huu wa majaribu tukimtafakari Bwana Yesu pale msalabani, chanzo cha faraja na wokovu.” Papa alisisitiza kuwa: “Tukiwa tunakabiliana na magumu tunayoyaona ulimwenguni na kuhisi mioyoni mwetu tudumu katika maombi kwa kushuhudua kila kila siku tumaini hilo linalotufanya kuwa chumvi ya dunia.” Kwa kuhitimisha Papa Francisko, amewakabidhi kwa maombezi ya Bikira Maria na Watakatifu Walinzi wa ona wawabariki wote kutoka moyoni mwake. Lakini hakukosa kuwaomba tafadhali wasali kwa ajili yake.