Papa akutana na Makamu rais wa Marekani,Bwana Vance.
Vatican News
Dominika asubuhi tarehe 20 Aprili 2025, muda mfupi baada ya saa5.30, katika nyumba ya Mtakatifu Marta, Papa Francisko alikutana kwa muda mfupi wa faragha na Makamu Rais wa Marekani, James David Vance. Hayo yalitangazwa na Ofisi ya Habari, Vatican ikieleza kuwa mkutano huo uliochukua dakika chache, ambao ulitoa fursa ya kubadilishana matashi mema ya Sikukuu ya Pasaka.
Akiwa safarini nchini Italia na familia yake, Vance vile vile alipokelewa asubuhi Jumamosi tarehe 19 Aprili 2025, na Kardinali Pietro Parolin, akiwa na Askofu Mkuu Paul Richard Gallagher, Katibu wa Mahusiano na Mataifa na Mashirika ya Kimataifa.
Mazungumzo yalikuwa muhimu , ambapo taarifa ilibanisha kuwa yalikuwa na dhamira ya pamoja ya kulinda haki ya uhuru wa kidini na uhuru wa dhamiri ilifanywa upya na kulikuwa na kubadilishana maoni juu ya hali ya kimataifa, hasa juu ya nchi zilizo na vita, mivutano ya kisiasa na hali ngumu ya kibinadamu, kwa umakini maalum kwa wahamiaji, wakimbizi na wafungwa.
Siku ya Ijumaa alasiri, Makamu Rais wa Marekani pia alishiriki, akiwa na mke wake na watoto watatu, Maadhimisho ya Mateso ya Bwana wetu Yesu Kristo katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro, mjini Vatican, yaliyoongozwa na Kardinali Claudio Gugerotti, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa kwa ajili ya Makanisa ya Mashariki