杏MAP导航

Tafuta

2025.04.09 Wafalme wa Uingereza watembelea Papa kwa faragha wakia nchini Italia katika kumbikizi lao la Ndoa. 2025.04.09 Wafalme wa Uingereza watembelea Papa kwa faragha wakia nchini Italia katika kumbikizi lao la Ndoa.  (Vatican Media)

Mfalme Charles na Malkia Camilla wamtembelea Papa kwa faragha katika kumbukizi yao ya ndoa

Papa Francisko alikutana kwa faragha na Wakuu wa Uingereza Mfalme Charles na Malkia Camilla tarehe 9 Aprili 2025 alasiri.Katika mazungumzo yao,Papa alipata fursa ya kutoa salamu na matashi mema kwa wafalme hao katika maadhimisho ya kumbukumbu ya ndoa yao na wakati huo walijibu kwa kumtakia heri ya kupona haraka afya yake.

Na Angella Rwezaula  - Vatican.

Wafalme wa Uingereza, Mfalme Charles na Malkia Camilla ambao walifika nchini Italia tangu tarehe 7 Aprili hadi tarehe  10 Aprili 2025, walipokelewa kwa faragha na Baba Mtakatifu Francisko alasiri tarehe 9 Aprili 2025 katika nyumba ya Mtakatifu Marta mjini Vatican ambapo Papa anaendelea kupata nafuu kwa majuma mawili, baada ya kulazwa katika Hospitali ya Gemelli jijini Roma. Kutoka kwa Papa na Mfalme walibadilishana matashi mema ya pamoja kwa ajili ya kupona haraka. Hayo yalisemwa na Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican.

Ziara hiyo iliyofuatia kutembelea Bunge la Italia, ilichukua takriban dakika ishirini na ilijumuisha ubadilishanaji wa zawadi binafsi. Waliokuwepo ni Katibu  wa Kibinafsi wa Wafalme hao, Sir Clive Alderton  na Naibu Katibu Binafsi wa Mfalme, Belinda Kim. Kwa njia hiyo katika mazungumzo yao, Papa alipata fursa ya kutoa salamu za heri kwa wafalme hao katika hafla ya maadhimisho ya kumbukizi ya harusi yao na wao kujibu kwa kumtakia heri apone haraka. Ziara hii ya mwisho ni marejeo ya hali ya kiafya ya Mfalme huyo ambaye vile vile alilazwa hospitalini mwishoni mwa Machi kutokana na athari za matibabu dhidi ya saratani iliyogunduliwa mwaka mmoja uliopita.

Taarifa za awali kutoka Jumba la kifalme Buckingham

Jumba la Kifalme la Buckingham lilikuwa limetangaza mkutano rasmi na Papa mwanzoni mwa Machi, wakati Papa Francisko alikuwa amelazwa hospitalini kwa siku chache kutokana na nimonia ya pande mbili, ikieleza kwamba Wafalme wa Uingereza wangetumia fursa hiyo ya kwanza ya safari yao nchini Italia hadi Vatican ili kusherehekea kumbikizi yao pamoja na Papa. Ujumbe uliofuata wa tarehe 24 Machi 2025 uliwasiliana kwamba Mfalme Charles III na mkewe hawatamwona tena Papa kutokana na mahitaji yanayohusiana na kupona kwake. “Wakuu wao, wanamtakia kila la heri Papa kwa ajili ya kupona kwake na wanatazamia kuzuru mjini Vatican mara tu atakapopata nafuu,” walikuwa wameandika

Mkutano wa kumtangaza Newman kuwa mtakatifu

Hii ni nia ambayo wanandoa hao waliweza kueleza ana kwa ana, wakati wa mkutano uliofanyika alasiri ya Jumatano 9 Aprili 2025. Mfalme Charles III, pamoja na kuwa mfalme wa Uingereza, pia kama inavyojulikana, ni mkuu wa Kanisa la Kianglikani. Mnamo mwaka wa 2019, kabla ya kutangazwa Mtakatifu Kardinali John Henry Newman, Mwingereza wa kwanza kutangazwa Mtakatifu katika zaidi ya miaka arobaini, Mkuu wa Wales wa wakati huo alitia saini nakala katika Gazeti la Osservatore Romano, akiita tukio hilo "sababu ya sherehe sio tu nchini Uingereza na sio tu kwa Wakatoliki, bali pia kwa wale wote wanaojali maadili yake." Mfalme Charles kisha alishiriki katika sherehe mjini Vatican tarehe 13 Oktoba 2019, na mwisho wake alisalimiana na Papa Francisko na ujumbe kutoka Uingereza. Wakuu wawili hao walikuwa tayari wamekutana tarehe 4 Aprili 2017, wakati wa ziara yake mjini Vatican.

Safari ya kwenda Italia

Katika siku hizi tatu za ziara, wafalme wa Uingereza walikutana na Rais wa Jamhuri Sergio Mattarella, Waziri Mkuu, Giorgia Meloni. Mfalme aliweza kuzungumza na Bunge lililokusanyika huko Montecitorio.

Mfalme Charles na Malkia Camilla
10 Aprili 2025, 10:10