Mtakatifu Maria Mkuu,masifu ya jioni ya makardinali na sala za watu kwa ajili ya Papa
Jioni ya Dominika 27 Aprili 2025 kulikuwa na maandamano ya Makardinali,waliofika katika Mikutano mikuu kwa mtazamo wa uchaguzi baada ya kifo cha Papa Francisko, walitembelea kaburi la Papa na kuadhimisha Masifu ya pili ya jioni,yaliyoongozwa na Kardinali Makrickas.Zaidi ya watu elfu 20 wamekuwa kwenye foleni tangu asubuhi ya leo ili kumsalimia Papa,kusali mbele ya jiwe lake la kaburi na kutoa heshima za maua katika kaburi hilo.
Na Angella Rwezaula - Vatican
Katika Dominika ya Pili ya Pasaka, ambayo ni Dominika ya Huruma ya Mungu, tarehe 27 Aprili 2025, washiriki wa Baraza la Makardinali walikwenda kwenye Kanisa kuu la Kipapa la Mtakatifu Maria Mkuu kutoa heshima zao kwa Baba Mtakatifu Francisko kwenye kaburi lake lililofunguliwa kwa umma tangu saa 1 asubuhi ya leo.
Kisha walikusanyika kwa pamoja katika masifu ya pili ya jioni, yaliyoongozwa na Mkuu wa Kanisa la hilo, Kardinali Rolanda Makrickas.
Nyuma yao, kulikuwa na makundi ya wamini walijumuika, huku wengine wakiendelea kuwasili wakati wa sherehe hizo kwa ajili ya kutoa heshima zao kwa Papa Francisko. Takriban watu elfu ishirini walikuwa tayari wametembelea kaburi hilo tangu asubuhi na mapema.
Waamini wakitoa heshima
27 Aprili 2025, 19:49