Ishara ya uwepo katika kipindi cha hali halisi ya mitandaoni
Andrea Tornielli
Ushiriki usio tarajiwa wa Papa Francisko wakati wa hitimisho la maadhimisho ya kiliturujia ya Jubilei iliyojikita kwa ajili ya wagonjwa na ya Ulimwengu wa kiafya, unawakilisha ujumbe wa kina sana. Hata wakati ambao hali halisi ya mitandaoni, katika kipindi ambacho tunaamini kuweza kushiriki yote tukibaki nyuma ya skrini ya Komputa, lakini uwepo kimwili ni muhimu sana. Kuwepo kama mtu, kupata ugumu wa kusafiri, wa kutoka, wa kusubiri; wa kufanya uzoefu mgumu wa kutembea, wa kukaribia wengine, wa kutokwa jasho, kupigwa jua au katika anga la wazi, ni mantiki ya kukutana na mtazamo wa wale walio karibu nasi, uzoefu wa kuwa na wengine, na kuwa sehemu ya watu wa mahujaji.
Katika ishara ambayo haikutangazwa, Mfuasi wa Petro, anatufundisha kuwa hakutakuwepo kweli na kamwe kinachoweza kubadilisha uwepo wa kimwili, yaani kuwepo kamili. Kutoka nje kwa Papa katika Jukwa la Uwanja wa Mtakatifu Petro kwa hivyo, jambo lenyewe ni ujumbe muhimu zaidi kuliko neno lolote: licha ya sauti ambayo bado dhaifu, licha ya mirija ya oksijeni aliyo nayo, lakini alitaka kuwa hapo.
Kuna maana nyingine ya pili: Papa Francisko alichagua kwa mara ya kwanza baada ya mwisho wa kulazwa Hospitalini Gemelli, katika maadhimisho ya Jubilei ambayo anahisi kwa namna ya pekee kuwa karibu: ile ambayo imejikita kwa wagonjwa, ambao wanateseka na kwa wale wanaowahudumia wanaoteseka. Hata kama hatari imepita, Papa Francisko bado anaendelea na kupumzika na matibabu ambapo lakini bado anaonesha ishara za ugonjwa. Ni mdhaifu kati ya wadhaifu ambaye hakukosa kushiriki “Jubilei yake, kwa kuungama katika Basilika na kupita katika Mlango Mtakatifu kama wanavyofanya maelfu na maelfu ya watu kila siku. Mlango ule ambao Papa alikuwa ameufungua usiku wa Noeli, na ambao Jana (6 Aprili) amepita kirahisi kama mhujaji ambaye bado anaendelea kubeba matokeo ya nimonia.
Hatimaye kutoka nje kwa kushtukiza Dominika asubuhi, kunatueleza juu ya uhusiano wa Mchungaji na zizi lake, Askofu na watu wake. Licha ya kuendelea kupona, licha ya maonyo ya madaktari, Papa Francisko hakukosa kukutana na watu, hata kama anatambua hatari inayoweza kutokea kwa ajili ya afya yake. Kwa kufanya hivyo kunatueleza kuwa hata ikiwa wakati mwingine licha ya hali ambayo inaweza kutokea, ya ì muktadha wa kutazama kupitia vyombo vya habari na mtandaoni kwa sababu ya kulazwa, au wakati wa karantini katika kipindi cha janga la Corona, au kutowezekana kusafiri, mkutano wa uwepo halisi, hauwezi kubadilishwa. Kwa sababu kama alivyokuwa amesema karibu mwaka mmoja uliopita kwamba: “Upendo unahitaji utekelezaji, upendo unahitaji kutolewa, wa kukutana na unahitaji muda na nafasi ya kutoa: hauwezi kupunguzwa katika maneno mazuri au picha katika skrini…” Na hii inatosha hata ya upendo wa Papa kwa ajili ya watu wa Mungu ambao daima “amezungumza hata kwa ishara na upole.