杏MAP导航

Tafuta

2025.03.20  Wanadiplomasia wa  Afrika wasali kwa ajili ya Papa Francisko. 2025.03.20 Wanadiplomasia wa Afrika wasali kwa ajili ya Papa Francisko. 

Wanadiplomasia wa Kiafrika wamwombea Papa,Turkson:Mungu amrudishie afya yake haraka!

Mabalozi wa Afrika waliopewa kibali kuwakilisha nchi zao mjini Vatican,tarehe 20 Machi 2025 walishiriki Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya kuombea uponyaji wa Papa iliyoadhimishwa kwenye Groto za Vatican.Mwaliko wa Kardinali Turkson ulikuwa ni kuweka"tumaini hai licha ya majaribu ya maisha."

Vatican News

Shukrani kwa miaka kumi na miwili ya Upapa wake na sala zilizoelekezwa kwa Baba Mtakatifu Francisko kwa ajili ya kupona haraka: sala zote zilizoinuliwa kutoka katika  Kikanisa cha Hungaria katika Groto za Vatican za Kanisa kuu la Mtakatifu Petro, Alhamisi, tarehe 20 Machi 2025 na mabalozi wa Afrika walioidhinishwa kuwakilisha Nchi zao mjini Vatican. Wanadiplomasia hao walikusanyika  kwa ajili ya Ibada ya Misa Takatifu iliyoongozwa na Kardinali Peter Kodwo Appiah Turkson, Chansela wa Vyuo vya Kipapa vya Sayansi na Sayansi ya Jamii. Baada ya kumuomba Mungu ampatie Papa nguvu zinazohitajika kutekeleza utume aliokabidhiwa, Kardinali huyo katika mahubiri  yake alipendekeza kutafakari kwa kina kuhusu kifungi cha Injili iliyosomwa ya tajiri na maskini Lazaro na kutoa mwaliko wa kuongoka mioyo na katika wema. "Tajiri alikuwa na mtihani wa kushinda, uwepo wa Lazaro maskini mlangoni pake. Mtihani ambao hakuweza kukabiliana nao," alisema Kardinali wa Ghana, huku akisisitiza jinsi ilivo sisi  "sote tuna mitihani ya kushinda katika maisha yetu."

wanaplomasia wa afrika wamwombea Papa
wanaplomasia wa afrika wamwombea Papa

Jubilei, chanzo cha matumaini

Kisha Kardinali pia aliwataka wanadiplomasia wa Afrika "kumwombea Baba Mtakatifu ili katika kukabiliana na majaribu haya, imani na matumaini yake kwa Mungu viweze kukua." Kadhalika katika Mwaka huu wa Jubilei," Kardinali Turkson alitafakari kuwa "Papa ameendelea kuhimiza matumaini. Jubilei hii ambayo ameiweka wakfu kwa matumaini, iwe chanzo cha matumaini kwake pia, katika Bwana," ndiyo ilikuwa matakwa ya mwisho ya Kardinali.

Wanadiplomasia wa Afrika wamwombea Papa
Wanadiplomasia wa Afrika wamwombea Papa

Mapendo ya Papa kwa bara la Afrika

Kando ya tukio hilo la misa, naye Balozi wa Cameroon anayewakilisha nchi yake mjini Vatican,  Bwana Antoine Zanga alimfafanua Baba Mtakatifu kuhusu ukaribu na mshikamano wa Kanisa katika  Bara zima la Afrika: “Tunamwombea sana Baba Mtakatifu Francisko zawadi ya afya na tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maombi  ya Baba Mtakatifu anayehitaji sala zetu daima. Tukiwa imara katika imani yetu." Mwanadiplomasia huyo aliendelea kusema: "tunamwilisha matumaini kwamba Bwana atamrejesha mtumishi wake kusimama na miguu yake ili kuendeleza utume aliokabidhiwa kwake na tunaomba kwamba Baba Mtakatifu mwenyewe awe na tumaini kwa Mungu. Ni Papa Francisko aliyefungua Jubilei hii ya matumaini. Tunatumaini kwamba anaweza kushiriki nasi na kwamba anaweza pia kuifunga,"alihitimisha.

 

 

21 Machi 2025, 14:27