Uwanja ule mtupu na mchungaji akishirikiana na ulimwengu
Andrea Tornielli
Miaka mitano imepita tangu Papa Francisko, akiwa peke yake, akitembea hadi ngazi za Uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro(tarehe 27 Machi 20220). Mvua ilikuwa ikinyesha jioni hiyo. Uwanja huo ulikuwa mtupu sana, ingawa mamilioni ya watu ulimwenguni kote walikuwa wakimtazama, huku wakiwa wametazama skrini zao za runinga, wakati walikuwa bado wamefungiwa kwa muda mrefu ndani ya nyumba zao huko wakiogopa virusi visivyoonekana ambavyo vilikuwa vikidai wathirika wengi, wakiwapeleka kwenye vitengo vya wagonjwa mahututi vya hospitali, bila jamaa na familia zao kuweza kuwaona, kusema kwaheri au hata kuudhuria mazishi. Kwa ishara hiyo, kwa sala hiyo, na kwa misa za kila siku kutoka katika kikanisa cha Mtakatifu Marta, Mrithi wa Petro alikuwa amejifanya kuwa karibu na kila mtu. Alikuwa amejumuisha kila mtu katika kumbatio la uwanja mtupu, katika baraka na Sakramenti Takatifu, katika ishara rahisi ya kubusu miguu ya Msalaba ambao ulionekana kama vile unalia kwa sababu ulifunuliwa na mambo ya jioni ya kuanza kwa majira ya kuchipua.
"Nilikuwa nikiwasiliana na watu. Sikuwa peke yangu wakati wowote…”, Papa alisimulia hayo muda fulani baadaye. Pekee, lakini sio peke yangu. Kuombea ulimwengu uliopotea. Picha yenye nguvu, isiyoweza kusahaulika, ambayo iliashiria upapa. Katika tukio hilo Papa Fransisko alisema, akimwambia Mungu: “Unatuita tuchukue wakati huu wa majaribio kama wakati wa kuchagua. Sio wakati wa hukumu yako, lakini wa hukumu yetu: wakati wa kuchagua kile ambacho ni muhimu na kinachopita, kutenganisha kile ambacho ni muhimu na ambacho si muhimu.” Ni wakati wa kuweka upya dira katika mwendo wa maisha kuelekea Kwako, Bwana, na kuelekea kwa wengine.” Katika miezi iliyofuata angerudia kusema kwamba “hutoki kamwe katika hali mbaya kama hapo awali. Tunatoka tukiwa bora au tunatoka vibaya zaidi."
Miaka mitano baadaye, tukitazama huku na huko, haiwezekani kusema kwamba tumetoka vizuri zaidi, na ulimwengu unaotikiswa na vurugu za wababe wa vita, ambao unafikiria juu ya kuweka silaha tena badala ya kupambana na njaa. Hatuko tena katika karantini, na sasa hali imebadilika: Uwanja umejaa watu wanaoadhimisha Jubilei, lakini Askofu wa Roma hayupo sasa, akituombea na kwa amani kutoka katika chumba chake huko Mtakatifu Marta, akipona kutokana na kesi mbaya wa mapafu na nimonia. Lakini maelewano hayo hayajavunjwa. Na maneno yake kutoka wakati huo yanafaa zaidi kuliko hapo awali: hata leo, hasa leo, ni "wakati wa kuchagua kile ambacho ni muhimu na kinachopita."