Papa huko Gemelli yuko katika hali tulivu,hakuna mashambulizi mapya ya kwikwi
Siku ya Jumamosi jioni, tarehe Mosi Machi 2025, Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican iliripoti taarifa ifuatayo kuhusu Papa Francisko:
Hali ya kiafya ya Baba Mtakatifu iliendelea kuwa thabiti.
Alibadilisha kati ya uingizaji hewa usio na uvamizi wa mitambo na muda mrefu wa oksijeni ya ziada ya mtiririko wa juu, kwa kudumisha mwitikio mzuri wa kubadilishana gesi.
Baba Mtakatifu hana homa na haoneshi 'leukocytosis,' yaani idadi kubwa ya seli nyeupe za damu.
Vigezo vyake vya (haemodynamic)mwendo wa damu daima vimebakia imara; ameendelea kula peke yake na mara kwa mara amefanya mazoezi ya kupumua, ambayo anashirikiana kikamilifu.
Hajapata matukio yoyote zaidi ya (bronchospasm)kwikwi.
Baba Mtakatifu anaendelea kuwa macho na mwelekeo mzuri.
Alipokea Ekaristi Jumamosi alasiri, kisha akajitolea kusali.
Utabiri unabaki kulindwa.