Papa huko Gemelli,hali tulivu,upokeaji wa hewa ya mitambo umesimamishwa
Vatican news
"Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu zimesalia kuwa shwari leo hii; Papa hakuhitaji uingizaji hewa ya mitambo isiyo na uvamizi, lakini matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu tu; Hana homa.
Kwa kuzingatia ugumu wa vipimo vya kliniki, utabiri unabaki kulindwa.
Asubuhi ya leo Baba Mtakatifu alishiriki Ibada ya Misa Takatifu, pamoja na wale wanaomhudumia katika siku hizi za kulazwa, kisha akabadilishana mapumziko na sala."
Haya ndiyo yaliyoripotiwa katika taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican, jioni ya leo Dominika tarehe 2 Machi 2025, kuhusu afya ya Papa, Francisko ambaye amelazwa hospitalini Gemelli Roma tangu 14 Februari.
Hapakuwapo na matokeo ya moja kwa moja ya shambulio la (bronchospasm) kwikwi lililojitokeza la kipekee siku ya Ijumaa iliyopita. Walakini, inabaki hatari ya kukosoa na kwa sababu hiyo utabiri unabakia kuhifadhiwa.
Imesasishwa mwisho saa 1.30 usiku tarehe 2 Machi 2025.