Papa Hospitalini Gemelli:Usiku ulikuwa mtulivu kwa Papa,anaendelea na tiba
Vatican News
Baada ya usiku mtulivu, Papa anaendelea kupumzika. Hii ndilo sasisho la taarifa kuhusu hali ya afya ya Papa, aliyelazwa Hospitalini Gemelli Roma, tangu tarehe 14 Februari, iliyotolewa asubuhi ya leo tarehe 6 Machi 2025 na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican.
"Baada ya kuamka Papa aliendelea na tiba, miongoni mwake mazoezi hai ya viungo. Kama ilivyopangwa, baada ya hewa ya mitambo isiyovamia wakati wa usiku, asubuhi aliendelea na ile ya Oksjeni ya mtiririko wa juu ya kutumia pua."
Taarifa ya tarehe 5 Machi
Katika taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican iliyotolewa jioni ya, Jumatano tarehe 5 Machi 2025, kuhusu afya ya Papa, ambaye amelazwa hospitalini tangu 14 Februari 2025 huko Gemelli Roma ilibanisha:
"Baba Mtakatifu pia alibaki thabiti leo bila kuwasilisha matukio ya kushindwa kupumua. Kama ilivyopangwa, wakati wa mchana, alipata matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu na uingizaji hewa wa mitambo usio na uvamizi utarejeshwa wakati wa usiku. Baba Mtakatifu ameongeza tiba ya viungo vya kupumua na mazoezi hai ya viungo. Alitumia siku nzima akiwa katika kiti cha sofa.
Kwa kuzingatia ugumu wa hali nzima ya kliniki, utabiri unabaki kuhifadhiwa. Asubuhi leo katika nyumba ya kibinafsi katika ghorofa ya 10, Baba Mtakatifu alishiriki katika ibada ya baraka ya Majivu Matakatifu ambayo aliwekwa juu ya kichwa chake na mshereheshaji, kisha akapokea Ekaristi. Baadaye alijitolea kwa shughuli fulani za kazi ndogo ndogo. Pia asubuhi alimpigia simu Padre Gabriel Romanelli, Paroko wa Familia Takatifu ya Gaza. Alasiri alibadilishana kazi kwa kupumzika."