杏MAP导航

Tafuta

Katekesi iliyoandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 5 Machi 2025 imekita mizizi yake katika: "Utoto wa Yesu.” Katekesi iliyoandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 5 Machi 2025 imekita mizizi yake katika: "Utoto wa Yesu.”   (Vatican Media)

Papa Francisko: Katekesi Kuhusu Yesu Tumaini Letu: Utoto wa Yesu

Katekesi iliyoandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 5 Machi 2025 imekita mizizi yake katika: “Utoto wa Yesu.” Jinsi ambavyo Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu walivyotaabika kumtafuta Mtoto Yesu hatimaye, wakamkuta akiwa ameketi katikati ya waalimu, wakimsikiliza na kumuuliza maswali. Huu ni mwaliko kwa waamini kutafakari hija ya Bikira Maria, ambayo kimsingi ilisheheni magumu na changamoto za maisha hadi pale aliposimama Mlimani Kalvari

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Ikawa baada ya siku tatu wakamwona hekaluni, ameketi katikati ya waalimu, akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Nao wote waliomsikiliza walistaajabia fahamu zake na majibu yake. Na walipomwona walishangaa, na mama yake akamwambia, “Mwanangu, mbona umetutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.” Akamwaambia, “Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. Huu ni mwendelezo wa Katekesi kuhusu: “Roho Mtakatifu na Bibi Arusi. Roho Mtakatifu anawaongoza watu wa Mungu kuelekea kwa Yesu, tumaini letu.” Katekesi iliyoandaliwa na Baba Mtakatifu Francisko, Jumatano tarehe 5 Machi 2025 imekita mizizi yake katika: Utoto wa Yesu.” Jinsi ambavyo Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu walivyotaabika kumtafuta Mtoto Yesu hatimaye, wakamkuta akiwa ameketi katikati ya waalimu, wakimsikiliza na kumuuliza maswali. Huu ni mwaliko kwa waamini kutafakari hija ya Mama wa Yesu, safari ambayo ilisheheni magumu na machungu ya maisha tangu pale Kristo Yesu alipotungwa mimba kwa uwezo wa Roho Mtakatifu, Bikira Maria alipomtembelea Elizabeti, Kristo Yesu alipozaliwa mjini Bethlehemu; baada ya Siku arobaini, Mtoto Yesu anatolewa Hekaluni na kwa wakati huu, wazazi wake Yesu walikuwa wamerejea tena kufanya hija ya kiroho mjini Yerusalemu Hii ni hija ya kiroho waliyoifanya baada ya kurejea kutoka Misri walikokuwa wamekimbilia ili kutoa hifadhi kwa Mtoto Yesu na kurejea tena mjini Nazareti baada ya kifo cha Mfalme Herode. Kristo Yesu alipokuwa kijana tayari alianza utume wake wa hadhara.

Hii ni picha iliyopigwa tarehe12 Februari 2025
Hii ni picha iliyopigwa tarehe12 Februari 2025   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Bikira Maria alikuwepo na kumfuatilia kwa ukaribu, kiasi kwamba, alionekana kuwa ni mhusika mkuu katika Arusi ya Kana ya Galilaya, hadi akamfuatia kwenye Njia yake ya Msalaba, akashuhudia mateso na kifo chake Msalabani. Baada ya ufufuko, Bikira alibaki na wanafunzi wa Kristo Yesu mjini Yerusalemu, wakiimarishana katika imani kwa kuendelea kusubiri ujio wa Roho Mtakatifu. Yote haya yanaonesha kwamba kwa hakika Bikira Maria alikuwa ni hujaji wa matumaini, akawa “Binti ya Mwanae mpendwa Kristo Yesu”, Mwanafunzi wa kwanza. Bikira Maria aliweza kumzaa Kristo Yesu, tumaini la walimwengu; akamlisha, akalea na kumkuza, Ndiye Mama aliyembeba Neno wa Mungu; akawa “Tabernakulo yake ya kwanza” kiasi kwamba, mawazo na utashi wake, ukawa ni katika utashi wa Mwenyezi Mungu, kiasi kwamba, Neno wa Mungu akamwilishwa ndani ya Bikira Maria. Hiki ni kielelezo cha umoja wa Neno wa Mungu, mwaliko kwa waamini kujibidiisha kulitafakari na kujitahidi kulielewa.

Bikira Maria alifanya hija ya matumaini katika maisha yake.
Bikira Maria alifanya hija ya matumaini katika maisha yake.   (Christian Media Center)

Baba Mtakatifu Francisko anasema, kupotea kwa Mtoto Yesu aliyekuwa na umri wa miaka kumi na miwili kuliwashtua sana wazazi wake, kiasi cha kuingiwa na huzuni, kwani hapo mwanzoni walidhani kwamba, alikuwa katika msafara, baada ya kutokumwona siku nzima, wakaanza kumtafuta kati ya jamaa na wenzao. Lakini waliporejea Hekaluni wakamkuta Hekaluni akiwa amezungukwa na waalimu akiwasikiliza na kuwauliza maswali. Kwa Bikira Maria na Mtakatifu Yosefu, Kristo Yesu alikuwa ni Mtoto ambaye alipaswa kutunzwa, lakini alionesha vipaji vilivyowashangaza wengi kiasi cha kujadiliana na waalimu kuhusu Maandiko Matakatifu. Bikira Maria alionesha kukasirika sana, lakini Kristo Yesu aliwajibu kwa upole “Kwani kunitafuta? Hamkujua ya kuwa imenipasa kuwamo katika nyumba ya Baba yangu? Lk 2:49. Nao hawakuelewa na neno hilo alilowaambia. Rej. Lk 2:50.

Bikira Maria Ni Kielelezo cha matumaini
Bikira Maria Ni Kielelezo cha matumaini   (Vatican Media)

Hili ni Fumbo la Mwenyezi Mungu aliyemwilishwa katika Neno, anapita ufahamu na uelewa wa binadamu. Wazazi wake walipania kumlinda Mtoto Yesu, chini ya mwamvuli wa upendo wao, lakini Kristo Yesu alitaka kuishi na kutekeleza wito wake wa kuwa ni Mwana wa Baba wa milele, kwa ajili ya huduma, huku akijizamisha katika Maandiko Matakatifu. Baba Mtakatifu Francisko anasema, na kwa maneno haya Bikira Maria, anafunga rasmi simulizi la Utoto wa Yesu unaowakumbusha waamini dhamana na wajibu wa Mtakatifu Yosefu katika malezi na makuzi ya Mtoto Yesu, yanayopata asili na chimbuko lake kutoka katika maneno ya Baba yake wa Milele. Bikira Maria na Mtakatifu Yoefu walisheheni sana matumaini, mwaliko kwa waamini kufuata nyayo za Kristo Yesu anaye wakirimia waja wake majibu ya upendo na maisha ya uzima wa milele.

Katekesi ya Papa Francisko

 

05 Machi 2025, 14:42