杏MAP导航

Tafuta

Papa anaendelea na matibabu,hospitalini Gemelli,Roma. Papa anaendelea na matibabu,hospitalini Gemelli,Roma. 

Papa Francisko amelala salama usiku kwa utulivu

Taarifa mpya kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari Vatican kuhusu afya ya Papa aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli iliyotolewa asubuhi ya leo Jumamosi tarehe 1 Machi 2025 imebainisha alivyolala salama usiku kwa utulivu na wakati wa kutoa taarifa hiyo alikuwa bado anapumzika.

Vatican News

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican kuhusu afya ya Baba Mtakatifu Francisko aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli tangu tarehe 14 Februari 2025, asubuhi, Jumamosi tarehe 1 Machi 2025 ilibanisha kuwa: “ Papa alilala salama usiku kwa utulivu na sasa bado anapumzika.”

Taarifa ya jana jioni

Katika taarifa iliyotolewa jana jioni, Ijumaa tarehe 28 Februari ilitangazwa kuwa Papa Francisko aliwasilisha, mapema alasiri, "shambulio la pekee la bronchospasm"(Kwikwi) ambalo "lilisababisha hata kutapika kwa kuvuta pumzi na kuzorota kwa ghafla kwa hali ya kupumua." Mara moja aliwekewa gesi ya mitambo isiyovamia "na kulikuwa na majibu mazuri kwenye kubadilishana gesi." Kwa kadiri inavyotambuliwa, thamani za ubadilishaji wa gesi ulirudi kama kawaida ya kabla ya shida iliyojitokeza. Daima alikuwa akisali na kuwa macho na mwelekeo mzuri.”

Katika  taarifa ya matibabu jana jioni pia ilibanishwa kwamba “Papa alishirikiana katika kupokea  matibabu. Itachukua takriban saa 24-48 kutathmini hali ya kiafya ya Papa baada ya shambulio hilo la pekee la bronchospasm, (yaani kwikwi).

01 Machi 2025, 09:06