Papa anaendelea kupata nafuu kidogo,upunguzaji wa oksijeni unaendelea
Vatican News
Ijumaa tarehe 28 Machi 2025, taarifa kutoka Ofisi ya vyombo vya habari, imesasisha kuhusu afya ya Papa Francisko kwamba:
"Hali ya afya ya Papa inaendelea kupata nafuu kwa mtazamo wa kupumua na mazoezi ya viungo na hata kwa upande wa kuzungumza. Kuna upunguzaji wa kutumia oksijeni ya mtiririko wa juu wa kutumia mirija ya pua kwa siku na kupunguzwa ile ya usiku. Vipimo vya damu ni vya kawaida kulingana na matokeo ya vipimo vilivyofanywa Jumatano tarehe 26 Machi. Papa anabadilishana siku kati ya matibabu ya dawa, sala, kupumzika kidogo na shughuli zake. Mabaraza yote ya kipapa yanamtumia hati. Hakuna ziara zozote maalum zilizopangwa. Amefuatilia mahubiri ya Kwaresima kwa mbali, asubuhi ya Ijumaa tarehe 28 Machi 2025. Tafakari ya Sala ya Malaika wa Bwana itatumwa kama ilivyokuwa Dominika zilizopitia. Papa alitaarifiwa juu ya tetemeko la ardhi nchini Myanmar na yuko anasali kwa ajili ya waathirika wengi. Kila siku anaadhimisha misa katika kikanisa cha Mtakatifu Marta.”