Papa anaimarika na anazidi kutumia oksijeni yenye mtiririko wa juu kidogo
Vatican News
Ofisi ya Waandishi wa Habari ya Vatican ilitangaza jioni hii tarehe 21 Machi 2025 ikitoa taarifa kuhusu hali ya Papa, ambaye amelazwa katika hospitali ya Gemelli Roma, tangu tarehe 14 Februari 2025 kuwa: “Hali ya kiafya ya Papa Francisko bado inaendelea kuimarika huku kukiwa na uboreshaji mdogo katika mifumo yake ya mazaoezi ya viungo na kupumua.”
“Siku za Papa zilipita kati ya tiba ya madawa, tiba ya mazioezi ya viungo, kupumua, maombi na kazi kidogo. Papa Francisko hakupokea wageni wowote. Wakati wa usiku hatumii tena uingizaji hewa ya mitambo na barakoa, lakini oksijeni ya mtiririko wa juu ka kutumia pua na wakati wa mchana hatumia mtiririko wa juu sana bali kidogo”.
Wakati huo huo: “katika Sala ya Maika wa Bwana ijayo imepangwa kufanywa kwa njia ile ile ya Dominika zilizopita. Ikiwa kuna maendeleo mapya, Ofisi ya Wanahabari Vatican itatoa sasisho Jumamosi. Hata hivyo Madaktari bado hawajatoa ishara yoyote juu ya kutoka hospitalini. Taarifa itakayofuata ya matibabu inatarajiwa si mapema zaidi ya Jumatatu.”