Papa Francisko Hospitalini Gemelli alilala vizuri wakati wa usiku
Vatican news
"Papa alilala vizuri wakati wa usiku, akaamka muda mfupi baada ya 2:00." Hii ni taarifa kuhusu hali ya afya ya Papa Francisko, aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli, Roma tangu Februari 14, iliyotolewa asubuhi ya leo, tarehe 5 Machi 2025, na Ofisi ya Vyombo vya Habari.
"Asubuhi hii Papa aliendelea na tiba yake na ya viungo vya kupumua. Kama ilivyopangwa, alihamia kutoka uingizaji hewa ya mitambo isiyovamia usiku hadi ya utiririshaji wa oksijeni ya juu kwa kutumia pua. Hali inaonekana kuwa thabiti, kila wakati katika muktadha wa hali tete."
Jana jioni Jumanne tarehe 4 Machi 2025, taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican ilibanisha: "Leo hali ya kimatibabu ya Baba Mtakatifu iliendelea kuwa shwari. Hakuwasilisha matukio ya kushindwa kupumua au (bronchospasm)kupumua papo hapo. Amebaki bila homa, daima akiwa macho, akishirikiana katika tiba na mwelekeo.
Asubuhi ya leo alibadilishiwa tiba ya oksijeni ya mtiririko wa juu na akafanyiwa mazoezi ya kupumua. Leo usiku, kama ilivyopangwa, atapewa hewa ya mitambo isiyovamia hadi kesho asubuhi. Utabiri unabaki kuhifadhiwa.
Wakati wa mchana alibadilishana na muda wa kusali na kupumzika na asubuhi ya leo alipokea Ekaristi."
Sasisho saa 9.10 alasili Jumatano 5 Machi 2025.