Papa alilala salama usiku mzima
Vatican News
“Papa Francisko alipumzika vizuri usiku mzima.” Ndiyo taarifa iliyotolewa katika taarifa kwa waandishi wa habari asubuhi ya tarehe 3 Machi 2025, katika Ukumbi wa Habari wa Vatican, kufuatia na hali halisi ya afya ya Papa aliyelazwa katika Hospitalini ya Gemelli, Roma tangu tarehe 14 Februari 2025.
Baadaye ilitolewa taarifa kuwa "Papa Francisko, baada ya kuamka, alipata kifungua kinywa na kuanza matibabu ya siku hii. Jioni ya leo kutakuwa na sasisho jipya la matibabu juu ya hali yake na vipimo."
Katika taarifa iliyotolea jana jioni, tarehe 2 Machi 2025 ilibainisha kuwa: "Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu zimesalia kuwa shwari leo hii; Papa hakuhitaji uingizaji hewa ya mitambo isiyo na uvamizi, lakini matibabu ya oksijeni ya mtiririko wa juu tu; Hana homa. Kwa kuzingatia ugumu wa vipimo vya kliniki, utabiri unabaki kulindwa. Asubuhi ya leo Baba Mtakatifu alishiriki Ibada ya Misa Takatifu, pamoja na wale wanaomhudumia katika siku hizi za kulazwa, kisha akabadilishana mapumziko na sala."
Sasisho la habari hii saa 7.22 mchana.