杏MAP导航

Tafuta

Mafuriko haya yamepelekea, watu zaidi ya 1,200 kukosa makazi ya kudumu na wengine wengi, hawajulikani mahali walipo! Hasara uiliyosababishwa na mafuriko haya inakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola za Kimarekani milioni 400. Mafuriko haya yamepelekea, watu zaidi ya 1,200 kukosa makazi ya kudumu na wengine wengi, hawajulikani mahali walipo! Hasara uiliyosababishwa na mafuriko haya inakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola za Kimarekani milioni 400.   (AFP or licensors)

Mafuriko Argentina: Watu 16 Wafariki Dunia; 1200 Hawana Makazi, Hasara M. 400

Mafuriko haya yamepelekea, watu zaidi ya 1,200 kukosa makazi ya kudumu na wengine wengi, hawajulikani mahali walipo! Hasara uiliyosababishwa na mafuriko haya inakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola za Kimarekani milioni 400. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican, Baba Mtakatifu anaonesha masikitiko yake makubwa kutokana na maafa haya, awaombea wote walioguswa na janga hili.

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Taarifa kutoka nchini Argentina zinaonesha kwamba, zaidi ya watu 16 wamepoteza maisha kutokana na mafuriko, ambayo yameikumba Argentina, siku ya Jumatatu, tarehe 10 Machi 2025. Mafuriko haya yamepelekea, watu zaidi ya 1,200 kukosa makazi ya kudumu na wengine wengi, hawajulikani mahali walipo! Hasara iliyosababishwa na mafuriko haya inakadiriwa kuwa ni zaidi ya dola za Kimarekani milioni 400. Baba Mtakatifu Francisko katika ujumbe ulioandikwa kwa niaba yake na Kardinali Pietro Parolin, Katibu mkuu wa Vatican kwenda kwa Askofu mkuu Carlos Alfons Azpiroz Costa, O.P. wa Jimbo kuu la Bahía Blanca lililoko nchini Argentina, anaonesha masikitiko yake makubwa kutokana na maafa makubwa yaliyosababishwa na mafuko.

Mafuriko yamesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.
Mafuriko yamesababisha maafa makubwa kwa watu na mali zao.   (AFP or licensors)

Baba Mtakatifu anapenda kuonesha uwepo wake wa karibu kwa njia ya sala na sadaka yake kwa waathirika wa mafuriko haya. Watu waliopoteza maisha, wapate raha ya milele na wapumzike kwa amani. Mwenyezi Mungu aendelee kuwa faraja kwa familia zote zilizoguswa na kutikiswa na mafuriko haya. Mwenyezi Mungu mwingi wa huruma na neema, awakirimie nguvu na neema za kuanza ujenzi na ukarabati wa maeneo yaliyokumbwa na mafuriko. Bikira Maria Mama wa Huruma, apeleke sala za waamini mbele ya Mwanaye mpendwa Kristo Yesu, ili waathirika waweze kuonja upendo wake wa daima. Mwishoni, Baba Mtakatifu amewapatia baraka zake za kitume.

Mafuriko Nchini Argentina
11 Machi 2025, 14:49