Hospitalini Gemelli Papa Francisko amekuwa na usiku mtulivu
Vatican News
"Papa alipata usiku mtulivu na aliamka muda mfupi baada ya saa 2:00 asubuhi." Hivi ndivyo Ofisi ya Vyombo vya habari , Vatican ililipoti kwa wanahabari tarehe 7 Machi 2025 kuhusu hali ya Papa Francisko, ambaye amelazwa hospitalini katika Gemelli Roma tangu Februari 14.
Sala ya Rosari
Kulikuwa na hisia kubwa katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican jana usiku, Alhamisi tarehe 6 Machi 2025 wakati, kabla ya kusali Rozari kwa ajili ya afya ya Papa, sauti iliyorekodiwa kutoka hospitalini Gemelli ilitangazwa ambapo Papa “aliwashukuru watu kwa sala na ukaribu wao,” akizungumza kwa lugha ya Kihispania.
“Agradezco de todo corazón las oraciones que hacen por mi salud desde la Plaza, los acompaño desde acá. Que Dios los bendiga y que la Virgen los cuide. Gracias.”
“Ninawashukuru kutoka ndani ya moyo wangu kwa maombi yenu kwa ajili ya afya yangu katika Uwanja, ninawasindikiza kutoka hapa. Mungu awabariki na Bikira awalinde. Asante”
“I thank you from the bottom of my heart for your prayers for my health from the Square, I accompany you from here. May God bless you and the Virgin protect you. Thank you.”
Tarifa za tarehe 6 Machi
Taarifa iliyotolewa jioni ya Alhamisi tarehe 6 Machi 2025, katika Ukumbi wa Vyombo vya habari Vatican, kuhusiana na afya ya Baba Mtakatifu aliyelazwa tangu tarehe 14 Februari 2025, katika Hospitali ya Gemelli Roma: “Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu zimebaki kuwa shwari zikilinganishwa na siku zilizopita. Leo pia hajawasilisha matukio ya kushindwa kupumua. Baba Mtakatifu aliendelea na mazoezi ya kupumua na ya mwili yenye faida. Vigezo vyote vya mzunguko wa damu na vipimo vya damu vilibakia imara. Hakuwa na homa. Madaktari bado wanadumisha utabiri uliohifadhiwa. Kwa kuzingatia uthabiti wa hali halisi ya kliniki, taarifa itakayofuata ya matibabu itatolewa Jumamosi. Baba Mtakatifu leo hii alijikita na baadhi ya shughuli ndogo ndogo wakati wa asubuhi na mchana, alipumzika na kusali. Kabla ya chakula cha mchana alipokea Ekaristi.”