Hali thabiti ya Papa huko Gemelli,hakuna shida mpya
Vatican News
"Leo hali ya kimatibabu ya Baba Mtakatifu iliendelea kuwa shwari. Hakuwasilisha matukio ya kushindwa kupumua au (bronchospasm)kupumua papo hapo. Amebaki bila homa, daima akiwa macho, akishirikiana katika tiba na mwelekeo.
Asubuhi ya leo alibadilishiwa tiba ya oksijeni ya mtiririko wa juu na akafanyiwa mazoezi ya kupumua. Leo usiku, kama ilivyopangwa, atapewa hewa ya mitambo isiyovamia hadi kesho asubuhi. Utabiri unabaki kuhifadhiwa.
Wakati wa mchana alibadilishana na muda wa kusali na kupumzika na asubuhi ya leo alipokea Ekaristi."
Hayo ndiyo yaliyoripotiwa katika taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican jioni ya leo hii, Jumanne tarehe 4 Machi 2025, kuhusu hali ya afya ya Baba Mtakatifu, aliyelazwa hospitalini tangu tarehe 14 Februari 2025 katika Hospitali ya Gemelli, Roma.
Taarifa hii imesasishwa Jumanne saa 1:11, jioni saa za Ulaya na saa 3:00 usiku masaa ya Afrika Mashariki na Kati.