Ask.Mkuu Arellano Cedillo:Katika Maadhimisho ya Mtakatifu Yosefu,Tumwombee Papa
Vatican News
Askofu Mkuu Alejandro Arellano Cedillo, Mkuu wa Mahakama ya Rota Romana, wakati wa kutambulisha sala ya Rozari katika Uwanja wa Mtakatifu Petro jioni ya Jumatano tarehe 19 Machi 2025 kama mwendelezo wa sala ya kuomba uponyaji wa Papa Francisko, aliyelazwa katika hospitali ya Gemelli Roma tangu tarehe 14 Februari 2025 alisema kuwa ““Ndugu zangu, mahujaji wa matumaini, tunakusanyika katika sala ili kusari Rozari Takatifu na kutafakari mafumbo ya maisha ya Yesu kwa mtazamo wa Bikira Maria. Kwa kuendelea aliongeza kusema kuwa “Picha ya Maria, Mama wa Kanisa iliyowekwa mbele ya Kanisa kuu la Vatican inakesha kwenye sala iliyoandaliwa na Sekretarieti ya Vatican na Jimbo la Roma, na kuhuishwa na Idara ya Toba ya Kitume, Vatican. Askofu Mkuu alikumbusha siku ya maadhimisho ya siku kuu ya Mtakatifu Yosefu, huku akitoa mwaliko wa Kanisa zima kusali kwa ajili ya afya ya Baba Mtakatifu.
Roho Mtakatifu, atusaidie katika udhaifu wetu
Makardinali, maaskofu, maaskofu wakuu, mapadre, wanaume kwa wanawake watawa wa Curia Romana na Jimbo la Roma walishiriki katika sala hiyo, pamoja na waamini waliokusanyika kumkabidhi Mrithi wa Petro kwa maombezi ya Bikira. Baada ya tafakari ya Mafumbo Matukufu na Sala ya Salamu Malkia kwa kuhitimisha na Litania ya Bikira Maria wa Loreto, Askofu Mkuu Arellano Cedillo aliomba karama ya Roho Mtakatifu “ili itusaidie katika udhaifu wetu, huku tukidumu katika imani, tukue katika upendo na kutembea pamoja katika lengo la tumaini lenye baraka.” Mwishowe, kusanyiko hilo uliimbwa wimbo wa kilatini “Oremus pro Pontifice” kusali kwa ajili ya Papa na Askofu mkuu akawaaga washiriki kwa baraka takatifu. Na wimbo wa mwisho kwa Bikira Maria ukaimbwa na Kwaya ndogo inayoongoza kila siku Rozari Takatifu.