Usiku wa Papa hospitalini Gemelli
Vatican News
"Papaalipitia usiku kwa utulivu, akaamka na kupata kifungua kinywa." Haya ndiyo yaliyotangazwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari, Vatican, Jumatano asubuhi tarehe 19 Septemba 2025. Jumanne alasiri tarehe 18 Februari 2025, Papa Francisko ambaye hali yake ya kimatibabu inaendelea kuwasilisha picha yenye utata, alifanyiwa uchunguzi kwa ya Xray ya kifua "iliyoagizwa na timu ya afya ya Vatican na timu ya matibabu ya Mfuko wa Hospitali ya A. Gemelli ambayo "ilionesha mwanzo wa nimonia pande mbili, ambayo "ilihitaji matibabu zaidi ya dawa", kwa mujibu wa taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya Habari ya Vatican.
Ujumbe kutoka kwa watoto wa saratani wa Hospitali ya Gemelli
Hata hivyo ujumbe kadhaa wa kumtakia ahueni ya haraka Papa kutoka kwa watoto waliolazwa katika Kitengo cha Saratani cha watoto hapo Gemeli wamemwandikia Baba Mtakatifu kwa kuchora michoro yao: "Kwa roho nzuri," Papa "asante kwa ukaribu anaohisi wakati huu na wanaomba, kwa moyo wa shukrani, kwamba tuendelee kumuombea," iliripoti katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari jioni tarehe 18 Februari 2025.
Maadhimisho ya Jubilei ya Mashemasi
Baba Mtakatifu kwa sasa anasumbuliwa na ugonjwa wa mkamba(Bronchitis) uliopelekea kulazwa tangu Ijumaa tarehe 14 Februari 2025 na kuendelea na vipImo vya kina zaidi. Wakati huo huo ikumbukwe Katekesi ya Siku ya Jumatano kuhusu Jubilei ya Mwaka 2025 ya Ukristo: Yesu Kristo Tumaini Letu, imefutwa. Wakati huo huo, Baba Mtakatifu amemteuwa Askofu mkuu Salvatore Rino Fisichella, Mwenyekiti mwenza, Baraza la Kipapa la Uinjilishaji wa Watu, kuadhimisha Ibada ya Misa Takatifu kwa ajili ya Mashemasi, Dominika tarehe 23 Februari 2025 kwenye Kanisa kuu la Mtakatifu Petro mjini Vatican, kuanzia majira ya Saa 3: 00 kwa Saa za Ulaya, sawa na Saa 5:00 kwa Saa za Afrika Mashariki na Kati. Maadhimisho ya Jubilei ya Mashemasi ni kuanzia tarehe 21 hadi tarehe 22 Februari 2025. Itakumbukwa kwamba, kuna makundi mawili ya Mashemasi ndani ya Kanisa.