杏MAP导航

Tafuta

Watu wa kiasili na wenyeji wa msitu wa Amazonia. Watu wa kiasili na wenyeji wa msitu wa Amazonia. 

Ujumbe wa Papa kwa Jukwa la Watu wa Asilia:Unyakuzi wa ardhi kwa upande wa mashirika ya kimataifa ni tishio kubwa!

Papa Francisko ametuma ujumbe tarehe 10 Februari 2025 kwa washiriki wa Kongamano la VII la watu wa Asilia, lililoandaliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo wa Umoja wa Mataifa(IFAD).Papa alisisitiza haki ya watu wa kiasilia kuhifadhi utambulisho wao wa kiutamaduni licha ya kutekwa na makampuni na serikali za kimataifa."Kutetea haki hizi sio suala la haki tu,bali pia kuhakikisha mustakabali endelevu kwa wote."

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Baba Mtakatifu Francisko Jumatatu tarehe 10 Februari 2025 ametuma ujumbe wake kwa washiriki wa Kongamano la VII la Watu wa Asilia, lililoandaliwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo la Umoja wa Mataifa(IFAD) tukio hilo, lililohudhuriwa na Askofu Mkuu Fernando Chica Arellano, Mwakilishi wa  Kudumu wa Vaticani  katika  Makao ya FAO, IFAD na WFP, na ambaye alisoma ujumbe huo wakati wa fursa hiyo  ujumbe wa Papa ulioelekezwa kwa Myrna Cunningham, rais wa Bodi ya Wakurugenzi wa Jukwaa hilo, Papa anaonesha shauku ya kutoa salamu kwa wote ambao wanashiriki  kwamba: “itakuwa nafasi muhimu ya mjadala, utafiti na kutafakari juu ya vipaumbele, wasiwasi na matarajio ya haki ya jumuiya asili. Mada iliyochaguliwa ya: “Haki ya Watu wa Kiasili ya Kujiamulia: Njia ya Usalama  na ukuu wa Chakula” Papa anabainisha kuwa    inatualika kutambua thamani ya watu wa kiasili, pamoja na urithi wa mababu wa ujuzi na mazoea ambayo kwa hakika hutajirisha familia kuu ya binadamu kwa kuipaka rangi na sifa tofauti za mila zao. Inafungua upeo wa matumaini katika saa ya sasa, yenye alama za changamoto kali na ngumu na mivutano mingi.

Haki ya kuhifadhi utamaduni na utambulisho

Utetezi wa haki ya kuhifadhi utamaduni na utambulisho wa mtu lazima uhusishe kutambua thamani ya mchango wao kwa jamii na kulinda uwepo wao na maliasili wanazohitaji ili kuishi. Hii inatishiwa pakubwa na ukuaji wa unyakuzi wa ardhi unaofanywa na mashirika ya kimataifa, wawekezaji wakubwa na mataifa. Haya ni mazoea ambayo yanaleta madhara, yanayoweka hatarini haki ya jamii kwa maisha yenye heshima. Ardhi, maji na chakula sio bidhaa rahisi, lakini ni msingi wa maisha na dhamana ya watu hawa na maumbile.

Jitihada zizae matunda na kuwa mvuto wa viongozi wa mataifa kwa kuchua hatua

Kwa hivyo, kutetea haki hizi sio tu suala la haki, lakini pia kuhakikisha mustakabali endelevu kwa wote. Kwa kuhuishwa na hisia ya kuwa wa familia ya kibinadamu, tutaweza kuhakikisha kwamba vizazi vijavyo vinanufaika na ulimwengu unaopatana na uzuri na wema ambao uliongoza mikono ya Mungu katika kuiumba. Papa Francisko anamwomba: “Mwenyezi Mungu kwamba jitihada hizi ziweze kuzaa matunda na kuwa mvuto kwa viongozi wa mataifa, ili hatua zinazofaa zichukuliwe ili familia ya binadamu itembee kwa umoja katika kutafuta manufaa ya wote, bila ya yeyote kutengwa au kuachwa nyuma.

Ujumbe wa Papa kwa Watu wa Asilia
10 Februari 2025, 14:04