杏MAP导航

Tafuta

Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa kwa ngazi ya kijimbo tarehe 11 Februari 2025 yananogeshwa na kauli mbiu “Na tumaini halitahayarishi” Rum 5:5, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu.” Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa kwa ngazi ya kijimbo tarehe 11 Februari 2025 yananogeshwa na kauli mbiu “Na tumaini halitahayarishi” Rum 5:5, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu.”  

Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko Kwa Siku ya 33 ya Wagonjwa Duniani 2025

Siku ya Wagonjwa Duniani, ilianzishwa tarehe 13 Mei 1992 na kuadhimishwa kwa mara ya kwanza kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Lourdes nchini Ufaransa kunako tarehe 11 Februari 1993. Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa kwa ngazi ya kijimbo tarehe 11 Februari 2025 yananogeshwa na kauli mbiu “Na tumaini halitahayarishi” Rum 5:5, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu.” Baba Mtakatifu anawaalika watu wote wa Mungu kuwa ni mahujaji wa matumaini!

Na Padre Richard A. Mjigwa, C.PP.S. – Vatican.

Siku ya Wagonjwa Duniani ni nafasi ya kutafakari kanuni maadili na utu wema; sera na mikakati ya shughuli za kichungaji kwa ajili ya wagonjwa na wazee, tayari kusoma alama za nyakati kwa kusikiliza na kujibu kilio cha wagonjwa na wale wanaoteseka. Hii ni siku maalum kwa ajili ya kukoleza uragibishaji na maadhimisho yanayokusudia kuwasaidia waamini kusali na kushiriki mateso ya wagonjwa; na kwa wagonjwa wenyewe kutolea mateso na mahangaiko yao kwa ajili ya ustawi, maendeleo na mafao ya Kanisa la Kristo Yesu na hatimaye, kuwaonjesha wagonjwa kuwa ni sura na ufunuo wa Kristo Yesu, anayeteseka kati pamoja nao. Hii ni siku inayopania kuamsha tena na tena huruma na upendo kwa wagonjwa, ili kuwatunza kwa mapendo ya dhati. Ni siku inayopania kukuza na kudumisha kanuni maadili, utu wema pamoja na haki msingi za wagonjwa, sanjari na kuangalia changamoto wanazokabiliana nazo wagonjwa na katika sekta ya afya kwa ujumla wake, ili kuweza kuzipatia majibu muafaka. Siku ya Wagonjwa Duniani, ilianzishwa na Mtakatifu Yohane Paulo II kunako tarehe 13 Mei 1992 na kuadhimishwa kwa mara ya kwanza kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Lourdes nchini Ufaransa kunako tarehe 11 Februari 1993. Maadhimisho ya Siku ya Wagonjwa kwa ngazi ya kijimbo tarehe 11 Februari 2025 yananogeshwa na kauli mbiu “Na tumaini halitahayarishi” Rum 5:5, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu.” Baba Mtakatifu anawaalika watu wote wa Mungu kuwa ni mahujaji wa matumaini katika mateso na mahangaiko ya binadamu.

Kauli mbiu "Na tumaini halitahayarishi, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu"
Kauli mbiu "Na tumaini halitahayarishi, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu"

Kwa kawaida Siku ya Wagonjwa Duniani, huadhimishwa kila baada ya miaka mitatu kwenye madhahabu ya Bikira Maria. Ni katika muktadha wa Maadhimisho ya Jubilei kuu ya Miaka 2025 ya Ukristo, maadhimisho haya yataadhimishwa tarehe 11 Februari 2026 kwenye Madhabahu ya Bikira Maria wa Chapi, huko Arequipa, nchini Perù “Virgine de Chapi, in Arequipa, Perù. Ikumbukwe kwamba, tarehe 11 Februari 2025 ni Jubilei ya Wagonjwa na Wahudumu katika Sekta ya Afya ngazi ya Jimbo. Tarehe 5 na 6 Aprili 2025 ni Jubilei ya Wagonjwa na Wahudumu katika Sekta ya Afya Kimataifa na tarehe 28 na 29 Aprili 2025 ni Jubilei ya Watu wenye Ulemavu. Ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko katika Maadhimisho ya Siku ya 33 ya Wagonjwa Duniani kwa mwaka 2025 yananogeshwa na kauli mbiu “Na tumaini halitahayarishi” Rum 5:5, lakini hutuimarisha wakati wa majaribu.” Baba Mtakatifu katika ujumbe huu, anakazia zaidi umuhimu wa kukutana, mateso na mahangaiko kama zawadi na kwamba, matumaini ni zawadi ya Mungu; mahangaiko ni sehemu muhimu sana ya kushirikishana na kutajirishana kwa kujikita katika maaana ya maisha, upendo na ujirani mwema. Baba Mtakatifu anawaalika wagonjwa na wale wote wanaoteseka kuwa imara. Kwa sababu fadhila ya nguvu huwezesha kushinda hofu, hata hofu ya kifo, na kukabiliana na majaribu; na madhulumu. Yamwandaa mtu kuwa tayari hata kujikatalia na kutoa sadaka ya uzima wake kwa ajili ya kutetea haki. Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu. Ulimwenguni mnayo dhiki, lakini jipeni moyo, mimi nimeushinda ulimwengu. Rej. KKK 1808.

Jubilei ya Wagonjwa na Wafanyakazi katika Sekta ya Afya 2025
Jubilei ya Wagonjwa na Wafanyakazi katika Sekta ya Afya 2025   (ANSA)

Kristo Yesu aliwatuma Mitume wake sabini na wawili kuwatangazia maskini kuhusu uwepo wa Ufalme wa Mungu. Rej. Lk 10: 1-9; kuwatangazia wagonjwa, licha ya shida na mahangaiko yao, kuwa ni fursa ya kukutana na Kristo Yesu. Katika magonjwa, mwanadamu anahisi udhaifu wake: kimwili, kisaikolojia na hata kiroho, lakini wakati huo huo, wagonjwa wanaonja pia uwepo wa Kristo Yesu anayeshiriki mateso na mahangaiko yao na kwamba, Mwenyezi Mungu kamwe hawaachi waja wake, lakini anaendelea kuwakirimia nguvu bila hata mastahili yao.  Ugonjwa unakuwa ni fursa ya kuleta mabadiliko chanya, kwa kutambua msingi thabiti wa matumaini ya maisha wakati wa dhoruba kali na kuwakumbusha kwamba, katika hali na mazingira kama haya, hawako peke yao, bali Mwenyezi Mungu daima ni faraja ya waja wake. Baba Mtakatifu Francisko anasema, mateso na mahangaiko ya mwanadamu ni zawadi ya matumaini na uaminifu wa Mungu katika Fumbo la Pasaka na kwamba, upendo wa Mungu daima utawaandama waja wake hata wakati wa majaribu na vikwazo katika maisha. Rej. Spe Salvi, 27, 31. Kristo Mfufuka anaendelea kutembea hatua kwa hatua na waja wake kama ilivyokuwa kwa wanafunzi wa Emau. Rej. Lk 24:13-53. Huu ni mwaliko kwa waamini kumshirikisha Kristo Yesu hofu na wasiwasi za maisha, hali ya kukata tamaa na hivyo kuwa tayari kusikiliza Neno lake, linalowapatia tena joto moyoni mwao na hivyo kuwa tayari kuutambua uwepo wake katika kuumega mkate, tukio linalowarejesha waamini kuonja ukaribu wa Kristo Yesu katika mateso na mahangaiko yao mahali popote pale wali

Mahujaji wa Matumaini
Mahujaji wa Matumaini

Huu ni mwaliko wa kutambua na kuthamini neema hii, kwa kuonesha ucheshi kwa wauguzi, moyo wa shukrani na uaminifu kutoka kwa mgonjwa, uso unaojali kutoka kwa daktari au mtu wa kujitolea; jicho la huruma na upendo kutoka kwa mwanandoa, mtoto, mjukuu au hata kwa rafiki. Baba Mtakatifu Francisko anasema, hii yote ni miali ya matumaini inayopaswa kutunzwa licha ya giza, tofauti na kwamba, haya yote ni chemchemi ya mafundisho yanayozama katika “sakafu” ya maana ya maisha, upendo na ujirani mwema kama ilivyokuwa kwa Msamaria mwema. Rej. Lk 10:25-37. Baba Mtakatifu anawakumbusha wagonjwa na wale wote wanaoteseka kwamba, wanao mchango muhimu sana katika Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 2025 ya Ukristo. Wao ni sehemu ya mahujaji wa matumaini kama yanavyobainishwa kwenye utenzi wa utu wa binadamu, wimbo wa matumaini. Huu ni wimbo wa matumaini shirikishi wa jamii nzima; wimbo wa faraja na nguvu, wenye uwezo wa kuleta mwanga wa faraja mahali unapohitajika. Kwa hakika, Mama Kanisa anamtolea Mwenyezi Mungu shukrani na Baba Mtakatifu Francisko anasema, anawakumbuka na kuwaombea wagonjwa; anapenda kuwakabidhi chini ya ulinzi na tunza ya Bikira Maria, Afya ya Wagonjwa. “Tunakimbilia ulinzi wako Mzazi Mtakatifu wa MUNGU usitunyime tukiomba katika shida zetu, utuokoe siku zote kila tuingiapo hatarini ewe Bikira Mtukufu na mwenye baraka Amina.”

Siku ya Wagonjwa 2025
10 Februari 2025, 13:31