Telegramu ya Papa ya rambirambi kwa waathirika wa ajali ya Bus huko Guatemala
Vatican News
Mauaji ya kutisha, zaidi ya mita 100 chini ya bonde na vifo karibia abiria 55 kati ya 75 katika ajali iliyotokea tarehe 10 Februari 2025, wakati wa kusafiri kwenye daraja nje kidogo ya mji mkuu wa Guatemala, Bus lililojaa liliruka kando ya barabara ya kitongoji cha Atlántida na likaanguka ndani ya mto wa maji na kuvunjika chini ya maji. Theluthi mbili za watu waliokuwemo ndani ya Bus hilo wakiwemo watoto walifariki na wengi wakijeruhiwa vibaya.
Mshikamano wa Papa
Ni katika mkutadha huo ambapo Baba Mtakatifu Francisko Ijumaa tarehe 14 Februari ameonesha kuhuzunika sana kufuatia na taarifa hiyo ya ajali na kutaka kueleza mshikamano wake kupitia telegramu iliyotiwa saini na Kardinali Pietro Parolin katibu wa Vatican , iliyoelekezwa kwa Askofu Mkuu Gonzalo de Villa y Vasquez, wa Mjini wa Santiago ya Guatemala. Katika maandishi hayo Papa, anatoa maombi yake kwa ajili ya mapumziko ya milele ya marehemu na rambirambi zake kwa familia, pamoja na wasiwasi wake mkubwa na matashi yake ya kupona haraka kwa majeruhi.
Maombelozi ya siku tatu ya kitaifa
Katika maelezo mapya ya tukio hilo kutoka kwa wazima moto, wanabainisha kuwa Bus hilo lililokuwa limejaa ambalo lilianhuka kutokana na kugongana kati ya magari kadhaa muda mfupi kabla ya mapambazuko ya siku ya Jumatatu. Rais Bernardo Arevalo wa Nchi hiyo alitangaza siku tatu za maombolezo ya kitaifa.