Ratiba za kipapa kwa mwezi Machi na Aprili 2025:Mafungo ya kiroho mjini Vatican
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na Askofu Mkuu Diego Ravelli, Mshehereshaji wa Liturujia za Kipapa, Jumatano tarehe 12 Februari 2025, amechapisha ratiba ya maadhimisho yanayotarajiwa kuongozwa na Baba Mtakatifu Francisko kwa mwezi Machi na mwanzoni mwa Aprili 2025.
Jumatano ya Majivu, 5 Machi
Katika ratiba hiyo ya maadhimisho ambayo Baba Mtakatifu anatarajia kwa siku zijazo, ni kuanzia na tarehe 5 Machi 2025 ambayo ni Jumatano ya Majivu. Katika Kanisa la Mtakatifu Anselmi saa 10.30 jioni, itafanyika maandamao ya toba hadi Basilika ya Mtakatifu Sabina ambapo saa 11.00 majira ya jioni, Misa Takatifu itafanyika kwa baraka na kupakwa majivu.
Jubilei ya Ulimwengu wa Watu wa kujitolea, 9 Machi
Tarehe 9 Machi, itakuwa ni Dominika ya Kwanza ya Kwaresima ambapo, katika Uwanja wa Mtakatifu Petro saa 4.30 majira ya asubuhi, itaathimishwa Misa Takatifu kwa ajili ya Jubilei ya Ulimwengu wa Watu wa Kujitolea
Mwanzo wa mafungo ya kiroho ya Papa na Curia Romana, 9-14 Aprili
Na tarehe hiyo hiyo 9 pia itakuwa ni mwanzo wa Mafungo ya kiroho ya Baba Mtakatifu na Wahusika wa Curia Romana itakayofanyika katika Ukumbi wa Paulo VI saa 11.00 jioni. Hadi tarehe 14 Machi 2025 itahitimishwa Mafungo ya kiroho ya Baba Mtakatifu na Wajumbe wa Curia Romana katika Ukumbi wa Paulo VI mjini vatican saa 3.00 asubuhi.
Jubilei ya wagonjwa na Ulimwengu wa Huduma ya Afya, 6 Aprili
Tarehe 6 Aprili 2025 itakuwa ni Dominika ya V ya Kwaresima ambapo katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican saa 4.30 itaadhimishwa misa Takatifu ya “Jubilei ya Wagonjwa na Ulimwengu wa Huduma ya Afya kwa Mwaka Mtakatifu.