Parokia ya Gaza imetuma video kwa Papa:Ulimwengu wote unasali kwa ajili yako
Na Salvatore Cernuzio – Vatican
Salamu na matashi mema, kwa njia ya video zimetoka kwa Padre Gabriel Romanelli, Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu na kwa wanaparokia huko Gaza, kwa ajili ya Baba Mtakatifu Francisko ambaye alilazwa tangu tarehe 14 Februari 2025, katika Hospitali ya A. Gemelli Roma. Katika ujumbe wao wanabainisha kuwa: “Mpendwa Baba Mtakatifu, kutoka hapa na wote ambao walikuwa kwenye Kanisa leo hata kama kuna baridi sana, lakini tunataka kukuonesha shukrani zetu, ukaribu wetu, na sala zetu. Ulimwengu wote unasali kwa ajili yako na una utambuzi kwako na wote tunatamani irudi afya yako."
Ukaribu na Papa
Wakiwa wamevalia majaketi na mitandio, wamejipanga mbele ya Altare chini ya picha ya Familia Takatifu inayoipatia jina la Kanisa hilo Waamini wa Kanisa la Gaza walimtumia Papa salamu kwa njia ya video chini ya sekunde 40, juzi ili kumtakia unafuu wa haraka na kumhakikishia maombi yao katika kipindi hiki kigumu cha kulazwa kwake katika hospitali ya Gemelli.
Hata hivyo ingekuwaje, baada ya yote, Paroko Gabriel Romanelli na watu wake, wanaopata hifadhi kati ya Parokia na chuo, wasiwe na ukaribu na Papa huyo ambaye, tangu kuzuka kwa vita, kati ya Palestina na Israeli, bila hata kukosa siku moja amekuwa akiwapigia simu kila saa 1 jioni ili kuwajulia hali? Simu za video vile vile zilizochukulia chini ya dakika moja kuuliza juu ya afya zao, hali ya maisha, walichokula siku hiyo, kutania na watoto na kutuma baraka zake, wakati mwingine hata kwa Kiarabu.
Simu ya Papa kutokea Gemelli.
Hata akiwa chumbani kwake Gemelli, katika siku za kwanza za kulazwa kwake, Papa Fransisko alimwita Paroko na Padre msaidizi wake, Yusuf Asad, wote wawili ni mapadre wa Shirika la Neno lililofanyika Mwili. Hata katika siku mbili za kwanza za kukaa hospitalini kwake licha ya matatizo yake ya kiafya na kukatika kwa umeme katika Jiji la Gaza - Papa alipiga simu mbili za video kupitia simu ya mkono wa mmoja wa washirika wake waliowekwa kwenye orofa ya kumi. Katika siku za hivi karibuni, Papa, pia kutokana na kuzorota kwa hali yake ambayo, ilionesha "maboresho kidogo"hakuweza kutimiza ahadi yake kwa marafiki zake huko Gaza. Alifanya hivyo juzi, kama ilivyoripotiwa na Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican, kwa kupiga simu kwa Familia Takatifu jioni. Na hasa, tunaposikia shukrani iliyopokelewa kwa njia ya video.
"Tunakutakia afya njema"
“Asante sana, tunakutakia afya njema, tunakuombea kila wakati,” mwanamume mzee kutoka Gaza anasikika akisema kwenye video hiyo. Pembeni mwake walikuwa wanawake, watoto na Masista Wamisionari wa Upendo. Wote kwa pamoja walimalizia kwa kusema pamoja : “Mungu akubariki kila wakati. Shukran, shukran!”.