Papa kwa Mfuko wa Gaudium et Spes:Ninyi ni sababu ya tumaini kwa watu wengi wanaoteseka na kukata tamaa
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Ijumaa tarehe 14 Februari 2025 alifurahi kukutana na Wajumbe wa Mfuko wa ‘Gaudium et Spes,’ alisema kuwa ni “katika Mwaka huu wa Jubilei ambao ndio kwanza tumeanza na ambao unatufanya sote kuwa mahujaji wa matumaini." Papa amlipenda kuwashukuru kwa kazi wanayoifanya, hasa kwa niaba ya maskini zaidi, kwa kufuata mafundisho ya katiba ya maridhiano ambayo walichukua jina lake na ambalo wanaliheshimu kwa matendo yao. Kwa maana hiyo, Mfuko na kazi zake zinaianya hati hiyo kuwa ya sasa, ambayo inapatana na roho ya Sinodi ya Kanisa, ambapo sisi sote tumeunganishwa katika Kristo, tukiunda udugu wa ulimwenguni pote, kama viungo vya Mwili wake ( 1Kor 12:12 na Rum 12:5). “
Baba Mtakatifu Francisko alisema kuwa “Muungano huu unapatikana kwa njia ya Roho Mtakatifu, ambaye ni Upendo, na unadhihirika katika mshikamano, hasa kwa wale wanaoteseka zaidi. Kukaa huku ndani ya Kristo kunatufanya tuwe familia, ndugu na tuwe na hadhi sawa. Na lishe ya familia hii inayokusanyika kula pamoja Dominika kwenye Misa ni Ekaristi. Tunaundwa mwili mmoja, kwa sababu tunakula mkate uleule (rej. 1Kor 10:17).
Papa alikazia akusema kuwa “Ni chakula cha kiroho kinachotolewa kwa kila mtu kwa kiwango sawa, na huturuhusu kuishi katika ushirika na Mungu na pamoja na ndugu zetu. Nguvu hii ya Roho Mtakatifu inatuongoza kuwa vyombo vya upendo wa Mungu unaotaka kuwafikia watu wote, bila ubaguzi.” Kwa hiyo, katika Mwaka huu Mtakatifu, Papa alipenda “kuwashukuru kwa sababu wao ambao, kupitia kazi zao, wadhaifu wanahisi kwamba Mungu anawajali na kuwafariji katika mateso yao. Yesu awabariki na Bikira Mtakatifu awalinde. “Na wasisahau kumuombea, pia Papa anawaombea.