杏MAP导航

Tafuta

Papa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya A. Gemelli, Roma. Papa anaendelea na matibabu katika Hospitali ya A. Gemelli, Roma.  (vincenzo livieri)

Papa huko Gemelli:hali bado ni tete lakini anapumua bila shida

Papa Francisko yuko macho,oksijeni inaendelea kutolewa,vipimo vya damu vimeboresha shukrani kwa utiaji wa damu mishipani,kuna kushindwa kidogo kwa figo ya awali.Leo alihudhuria Misa.Kutoka katika akaunti X,Papa anawashukuru watoto kwa maneno ya upendo na ukaribu aliyopokea,akisema alivutiwa na michoro na barua za watoto.Wengi wao walifikishwa Gemelli na wanafunzi wadogo kutoka shule za Italia.Misa na Rozari wamemwombea katika majimbo yote.

Vatican News.

Ofisi ya Habari ya Vyombo vya habari Vatican ilitoa taarifa  kuhusu matibabu  ya Baba Mtakatifu  Francika Dominika jioni tarehe 23 Februari 2025:

"Hali ya Baba Mtakatifu bado ni tete, lakini tangu jana jioni, hajapata matatizo zaidi ya kupumua.Alifanyiwa vipimo viwili vya seli nyekundu za damu zilizojilimbikizia na matokeo ya vipimo  vyake vya damu vimeongezeka. Thrombocytopenia(uwepo wa idadi ndogo za seli za damu)zinabaki thabiti; hata hivyo, baadhi ya vipimo vya damu vinaonesha kushindwa kidogo kwa figo, ambayo kwa sasa iko chini ya udhibiti. Anatumia mtiririko wa oksijeni kwa ajili ya kupumua.

"Baba Mtakatifu anaendelea kuwa macho na mwenye mwelekeo mzuri. Ugumu wa hali ya kliniki na wakati unaohitajika kwa matibabu ya madawa ili kuonesha matokeo ya dawa unahitajika  ili kuweza kutoa maoni fulani na  kwamba vipimo vya ubashiri unabakia kuhifadhiwa.

Asubuhi ya leo, katika ghorofa ya kumi, alishiriki katika ibada ya Misa Takatifu, pamoja na wale ambao wanamtunza kwa siku hizi za kulazwa hospitalini." Hizo ndizo taarifa zilizotolewa jioni hii.

Misa, maombi na msaada kupitia mitandao ya kijamii

Kwa siku nyingi, habari kuhusu Papa zimechochea harakati za sala na ukaribu kuelekeza Papa katika Makanisa  ulimwenguni. Na hata kwenye mitandao ya kijamii, sehemu kubwa za habari za uwongo, lakini vile vile hata mtiririko wa hiari wa machapisho umeanza kutoka kwa watumiaji ambao walitaka kutuma ujumbe wa kumuunga mkono na kumshukuru Papa (mara nyingi huambatana na picha za mikutano yao na Papa Francisko), wa majuto kwa wakati anapitia na pia wa kuhimiza kukusanyika pamoja na kusali kwa ajili yake.


 

23 Februari 2025, 19:55