Papa huko Gemelli,hali bado ni tete,lakini thabiti
Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican imesasisha kuhusu afya ya Papa:"hakuna matukio mabaya ya kupumua papo kwa hapo,vigezo vya damu ni thabiti.Uchunguzi wa vipimo uliratibiwa ambao ulifanywa kwa ufuatiliaji na picha ya X-ray kuhusu mkamba wa sehemu mbili.Ubashiri unabaki kuhifadhiwa."
Vatican News
Taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican Jumanne jioni, tarehe 25 Februari 2025 kuhusu afya ya Baba Mtakatifu Francisko aliyelezwa tangu tarehe 14 Februari katika Hospitali ya Gemelli, Roma imebainisha kuwa hajapata matatizo ya kupumua, na vigezo vyake vya damu bado ni thabiti. Utabiri unabaki kulindwa.
Papa alipokea Ekaristi na kuendelea na shughuli zake
Taarifa ya Ofisi ya Vyombo vya habari vya Vatican imebainisha jioni hii, saa 1:20, saa za Ulaya ambapo ni saa 3:20, masaa ya Afrika Mashariki na Kati iliongeza: “Jioni hii Papa alifanyiwa uchunguzi wa X-ray uliopangwa kwa ajili ya ufuatiliaji wa picha ya ugonjwa wa mkamba wa sehemu mbili na Utabiri unabaki kuhifadhiwa. Asubuhi ya Jumanne Februari 25, mara baada ya kupokea Ekaristi, aliendelea na shughuli zake za kazi."
25 Februari 2025, 19:56