Papa hospitalini Gemelli,hali inaboreka kidogo
Vatican News
Katika taarifa kutoka Ofisi ya Vyombo vya Habari vya Vatican iliyotolewa jioni hii, tarehe 24 Februari 2025 katika kusasisha hali ya afya ya Baba Mtakatifu ambaye amelazwa katika Hospitali ya Agostino Gemelli, Roma tangu tarehe 14 Februari 2025 inabainisha kuwa:
“Hali za kimatibabu za Baba Mtakatifu, katika umuhimu wake, zinaonesha kuboreka kidogo. Hata leo hii hapakuwa na matukio ya matatizo ya kupumua; baadhi ya vipimo vya maabara vimeboreka. Kufuatia na kushindwa kwa figo kidogo sio suala la kuwa na wasiwasi.
Anaendelea kupewa Oksijeni, ingawa asilimia ya mtiririko wa oksijeni imepunguzwa kidogo. Madaktari kwa kuzingatia ugumu wa picha ya hali ya kliniki, kwa busara bado hawatoi utabiri.
Asubuhi alipokea Ekaristi, na mchana aliendelea na shughuli zake kama kawaida. Jioni hii aliita Paroko wa Gaza kueleza ukaribu wake wa ubaba. Baba Mtakatifu Francisko anawashukuru Watu wote wa Mungu waliokusanyika katika siku hizi kumuombea afya yake."