Papa:“Hakuna majina kwa wazazi waliopoteza mtoto"
Vatican News
Hakuna hata maneno ambayo unaweza kutoa kwa jina kwa ajili ya mama au baba ambaye anapoteza mtoto. Mwanamke anayepoteza mme ni mjane. Mwanaume anayepoteza mke ni mgane. Mtoto anayepoteza wazazi ni yatima. Lakini kwa mzazi ambaye anapoteza mtoto, neno hakuna.”Ndivyo anaandika Papa Francisko katika kursa za “Piazza San Pietro,” yaani “Uwanja wa Mtakatifu Petro,” gazeti la kila mwezi linaloongozwa na Padre Enzo Fortunato(OFMConv) linalochunguza mada za imani, hali ya kiroho na maisha ya kila siku, likijibu - kama kila mwezi - kwa mojawapo ya barua zilizotumwa kwake. Ni ile ya mwanamke ambaye alipata maumivu makubwa zaidi: kuona mtoto wake akifa.
Uzoefu wa uchungu
Msiba wa Cinzia, mama wa Kirumi aliyefiwa na mtoto wake wa kiume mwenye umri wa miaka 21 katika ajali ya gari, ulimgusa Baba Mtakatifu. “Yesu, anayelia pamoja nasi, atapanda mioyoni mwetu majibu yote tunayoyatafuta,” huo ni ujumbe wa Papa, uliofafanuliwa sana siku zilizopita kabla ya kulazwa kwake hospitalini na ambaye, akimnukuu Mtakatifu Yohane Paulo wa Pili, anaandika kuwa: “Hakuna uovu ambao Mungu hajui jinsi ya kuteka mema zaidi yake”.
Michango katika gazeti
Kutoka katika kurasa za "Uwanja wa Mtakatifu Petro,"(Pizza San Pietro), Kardinali Charles Bo, Askofu Mkuu wa Jimbo la Yangon, anasimulia hali ngumu ya Myanmar, dhamana ya Kanisa na wito wa kudumu wa Papa kwa ajili ya amani katika nchi iliyokumbwa na migogoro.
"Mkutano Unaoponya" ni jina la mchango wa Sr Simona Brambilla, Mmisionari wa Upendo, Mwenyekiti wa Baraza la Kipapa la Mashirika ya Kitawa na Vyama vya Kitume, ambaye anaeleza jinsi ya uzoefu wa Mungu aliyepiga magoti yake anavyotugeuza kuwa kaka na dada wenye uwezo wa huruma na kukaribisha. Katika sehemu ya kiutamaduni, kwenye hafla ya Jubilei ya Wasanii, mahojiano na msanii Maurizio Cattelan alisema: "Uchochezi sio mwisho bali ni zana.”