Papa Francisko:Tuziombee nchi zilizo katika vita na tukumbuke watu waliokimbia makazi,Palestina
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Kama kawaida yake, Baba Mtakatifu Francisko katika Katekesi yake tarehe 5 Februari 2025 katika Ukumbi wa Paulo VI hakukosa kukumbuka nchi zilizogubikwa na migogoro na matokeo yake mabaya. Licha ya kuwa na mafua ambayo yalimzuia hasisome katekesi yake kwa kumkabidhi Padre Pierluigi Giroli, Mkuu wa ofisi ya Sekretarieti ya Vatican, Baba Mtakatifu alipenda hata hivyo “kutamka mwenyewe Wito kwa ajili ya Nchi ambazo zinateseka na vita”
“Na tunafikiria nchi zinazoteseka kwa sababu ya vita: Ukraine inayoteswa, Israeli, Jordan ... Kuna nchi nyingi zinazoteseka huko. Tunawakumbuka watu waliokimbia makazi yao huko Palestina na tunawaombea," Papa alisema.
Maombi kwa Mapadre katika Nchi Maskini au Vita-Katika Vita
Hata katika salamu zake kwa mahujaji wa Poland, Papa alitaja maeneo yaliyokumbwa na umaskini au vurugu, akiwahimiza "kuombea mapadre na watu waliowekwa wakfu ambao wanatekeleza huduma yao katika nchi maskini na zilizoharibiwa na vita," hasa "huko Ukraine, katika Mashariki ya Kati na katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo".
Salamu kwa mahujaji
Ninawakaribisha kwa moyo mkunjufu mahujaji wanaozungumza Kiitaliano. Kwa namna ya pekee, nawasalimia wanahija ya Jimbo la Mazara dya Vallo pamoja na Askofu Angelo Giurdanella; Ninawasalimu waamini wa Mtakatifu Angelo huko Esca, kituo cha Benedikto XVI cha Buccinasco na wanafunzi wa shule ya Mtakatifu Paolo ya Pogliano Milano. “Ninatumaini kwamba kutembelea makaburi ya Mitume kutachochea katika jumuiya zenu hamu mpya ya kuambatana na Kristo na kutoa ushuhuda wa Kikristo.”
“Hatimaye, mawazo yangu yanawaendea vijana, wagonjwa, wazee na wenye ndoa za hivi karibuni. Kama vile mtume Paulo anavyohimiza, ninawatia moyo muwe na furaha katika tumaini, hodari katika dhiki, mkidumu katika kuomba, mkizingatia mahitaji ya ndugu zenu ( Warumi 12:12-13). Baraka yangu kwa wote,” Papa alisema.