杏MAP导航

Tafuta

2025.02.07 KONGAMANO LA MIITI JIJINI MADRID HISPANIA 2025.02.07 KONGAMANO LA MIITI JIJINI MADRID HISPANIA 

Papa Francisko kwa Kongamano la Miito,Hispania:Wito ni kutambua mahitaji ya wengine!

Katika ujumbe wa Kongamano la siku tarehe 7-9 Februari 2025 kuhusu wito nchini Hispania,Papa anatoa mwaliko wa kufanya talanta zao zizae matunda daima.Ndiyo kusudi kuu la kuwepo,mahali popote Mungu anapowatuma,kuanzia ofisi za kazi na familia.Kongamano hilo linafanyika mjini Madrid na kuwaleta pamoja washiriki 3,000 kutoka majimbo 70 ya Hispania,wakisindikizwa na Maaskofu 65.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Katika ujumbe wa Baba Mtakatifu Francisko  kwa washiriki wa Kongamano la siku tatu kuanzia tarehe 7-9 Februari 2025 kuhusu wito nchini Hispania, alitoa mwaliko wa kutumia talanta zao zizae matunda na ndiyo kusudi la kuwepo mahali popote  ambapo Mungu anawatuma kupeleka utume wao katika kazi na katika familia zao. Baba Mtakatifu Francisko katika Ujumbe wake kwa washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Miito nchini Hispania, linaloongozwa na mada “Mimi ni kwa Ajili ya Nani? Mkutano wa Wale Walioitwa katika Utume,” kuanzia tarehe 7 hadi 9 Februari 2025 na aliwaalika“kustawisha mtazamo unaotambua mahitaji ya kaka na dada zenu.” Kongamano hilo linafanyika mjini Madrid kwa kuwaunganisha pamoja washiriki 3,000 kutoka majimbo 70 ya Hispania, wakisindikizwa na Maaskofu 65.

Kongamano la miito huko Madridi
Kongamano la miito huko Madridi

Washiriki hao wanaowakilishwa, miongoni mwao kuna Harakati na vyama vya walei 54, mashirikia  120 ya kitawa , na mashirika mengine 250 yanayoendeshwa na utume wa kimisionari na takriban theluthi moja ya washiriki  hao wako chini ya umri wa miaka 35. Kongamano hili la siku tatu linaadhimisha hitimisho la mpango wa kichungaji wa Maaskofu wa Hispania, ulioanzishwa mwaka 2021. Hata hivyo mada hiyo inajikita na swali lililoulizwa na Papa Francisko katika Hati yake ya Kitume ya Christus Vivit (n.286), iliyochapishwa kufuatia Mkutano Mkuu wa XV  wa Sinodi ya Vijana, kwa kuongoza na kauli mbiu: “Imani,na Mang’amuzi ya miito.”

Jaribu kuu ni upendo

Akitumia simulizi la kibiblia la kijana tajiri, Papa Francisko alitafakari jibu la Kristo kwa swali la jinsi ya kupata uzima wa milele. Alisisitiza kwamba sisi sote ni mawakili wa karama za neema na asili ambazo Bwana ametupatia. Vipaji vyetu lazima viwekezwe na vitoe riba; mali zetu lazima zigawanywe ili manufaa yawafikie wengine." Papa alisisitiza kwamba “mema tunayotafuta hayawezi kupatikana  kwa kutimiza mahitaji au kufikia malengo tu. Hata kama tutajitahidi kufanya kila kitu kuanzia umri mdogo, badala yake kitu muhimu kitakosa sikuzot lakini zawadi kamili ya sisi wenyewe katika kumfuata Yesu ni katika jaribu kuu la upendo.” Baba Mtakatifu  pia alikumbuka mafuriko makubwa yaliyoikumba Hispania mwishoni mwa Oktoba 2024 akiakisi vitendo vingi vya ujasiri na mshikamano vilivyofuata. Papa alisisitiza kwamba wengine ndio kusudi dhahiri la maisha yao. Kisha  alitofautisha yule kijana tajiri ambaye alishindwa kuwekeza katika utume muhimu ambao Mungu aliwaita pamoja na wale ambao walichukua hatua ya ajabu za kusaidia waathiriwa wa maafa, kuwakaribisha wahamiaji, au kusaidia wakati wa mlipuko mbaya wa volkano ( Palma.)

Kongamano la miito Madridi
Kongamano la miito Madridi

Papa alihimiza dhidi ya kufuja mali zao za  kimwili na za kiroho, akionya kwamba zinaweza kuwatenganisha na wengine na kutoka kwa Mungu.  Badala yake, aliwatia moyo watu wafikie hatua ambapo hawawiwi  na chochote sisi kwa sisi ila upendo. Alikazia zaidi uhitaji wa kumpeleka Mungu katika sehemu zote za maisha, akisema, “Huu ndio wito wetu.” Papa Franciko alipuuza dhana kwamba rasilimali za mtu hazitoshi, na kuwakumbusha waamini kwamba ingawa mitume walikosa "dhahabu na fedha," baada ya kupokea Roho Mtakatifu, walitambua mahitaji ya maskini na kuitikia zaidi ya matarajio. Badala ya kutoa sadaka, walimwalika yule aliyepooza hekaluni (rej. Mdo. 3:1-8) kuwatazama, kushuhudia umaskini wao, na, mara walipopata usikivu wake, ainuke kutoka katika mateso yake.

Kongamano lilifunguliwa kwa salamu kutoka kwa Askofu Luis Argüello, Rais wa Baraza la Maaskofu Hispania (CEE); Kardinali José Cobo, Askofu Mkuu wa Madrid; Askofu Mkuu José Manuel García Cordeiro wa Braga, Msimamizi wa Miito na Vijana katika Shirikisho la Mabaraza ya Maaskofu wa Ulaya (CCEE); na Balozi wa Vatican nchini Hispania, Askofu Mkuu José Manuel García Cordeiro. Tukio hilo lilianza kwa uwasilishaji wa hati ya mfumo wa awali, matokeo ya juhudi za pamoja. Siku ya kwanza ilihitimishwa kwa mkesha wa maombi ulioongozwa na Askofu Carlos Escribano, Rais wa Tume ya Maaskofu kwa Walei, Familia na Maisha. Jumamosi ilikuwa ni  majadiliano juu ya mada nne muhimu: Neno, Jumuiya, Somo, na Misheni. Takriban warsha sitini metarajiwa kwa  kila mada, na kuhitimishwa na ripoti ya mwisho ya muhtasari wa maarifa na mapendekezo ya Kongamano hilo.

Ujumbe wa Papa Kongamano la miito Hispania
08 Februari 2025, 12:57