Papa Francisko,katekesi ya Jubilei:Mungu anaanza safari yake kwa unyenyekevu
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Katika mzunguko wa katekesi ya Jubilei ya 2025 inayoongozwa na mada ya “Yesu Kristo Tumaii letu: Utoto wa Yesu”, Jumatano tarehe 12 Februari 2025, Baba Mtakatifu Francisko amejikita na sehemu ya 5 “Amezaliwa kwa ajili yenu Mwakozi, ambaye ni Kristo Bwana (Lc 2,11). Kuzaliwa kwa Yes una kufika kwa wachungaji. Kabla ya tafakari limesomwa somo kutoka katika Injili yaLuka(Lc 2,10-12):“Malaika akawaambia,(Wachungaji) Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa, kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana.Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng'ombe.” Baada ya somo hilo, kwa waamini na mahujaji waliokusanyika katika Ukumbi wa Paulo VI mjini Vatican, Baba Mtakatifu aliwasalimia na kuwaeleza kuwa katika mchakato wa Jubileio ya Katekesi kuhusu Yesu, ambaye ni tumaini letu, leo tunajikita na tukio la kuzaliwa kwake Betlehemu. Papa aliongeza akiomba samahani ili katekesi iliyoandaliwa isomwe na Padre Pierluigi Giroli, wa Shirika la Warosimini na Afisa wa Sekretarieti ya Vatican, sababu Papa bado hawezi kusoma bali anayo matarajio ya wakati ujao.
Akianza kusoma katekesi hiyo alisema "Mwana wa Mungu anaingia katika historia akiwa msafiri mwenzetu na alianza kusafiri angali katika tumbo la uzazi la mama. Mwinjili Luka anatuambia kwamba mara tu alipochukuliwa mimba alitoka Nazareti hadi nyumbani kwa Zekaria na Elisabeti; na kisha, mara mimba ilipotimia, alitoka Nazareti hadi Bethlehemu kwa ajili ya sensa. Maria na Yosefu walilazimika kwenda katika jiji la Mfalme Daudi, ambako Yosefu pia alizaliwa. Masiha aliyengojewa kwa muda mrefu, Mwana wa Mungu Aliye Juu Zaidi, alijiruhusu kuhesabiwa, yaani, kuhesabiwa na kuandikishwa, kama raia mwingine yeyotjuu ya kuzaliwa kwa Yesu katika "wakati unaoweza kutambulika kwa usahihi" na "mazingira ya kijiografia yaliyooneshwa kwa usahihi", ili "ulimwengu na ukweli ugusane" (Benedikito XVI, Utoto wa Yesu, 2012, 77). Mungu anayekuja katika historia hadhoofishi miundo ya ulimwengu, lakini anataka kuwaangazia na kuwaumba upya kutoka ndani. Bethlehemu maana yake ni "nyumba ya mkate." Hapo siku za kjifungua kwa Maria zilitimia na huko Yesu alizaliwa, mkate ulioshuka kutoka mbinguni ili kushibisha njaa ya ulimwengu (Yh 6:51). Malaika Gabrieli alikuwa ametangaza kuzaliwa kwa Mfalme wa Kimasiha katika ishara ya ukuu: “Tazama, utachukua mimba ndani ya tumbo lako la uzazi na kuzaa mtoto mwanamume, nawe utamwita jina lake Yesu. Yeye atakuwa mkuu na ataitwa Mwana wa Aliye Juu Zaidi; “Bwana Mungu atampa kiti cha enzi cha Daudi, baba yake, naye atatawala juu ya nyumba ya Yakobo hata milele, na ufalme wake hautakuwa na mwisho” (Lk 1:32-33).
Hata hivyo, Yesu alizaliwa kwa njia ambayo haikuwa na kifani hata kidogo kwa mfalme. Kiukweli, “wakiwa huko, siku zake za kujifungua zikafika. “Akamzaa mwanawe mzaliwa wa kwanza, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni” (Lk 2:6-7). Mwana wa Mungu hakuzaliwa katika jumba la kifalme, lakini nyuma ya nyumba, katika nafasi ambayo wanyama wanaishi. Kwa hivyo Luka anatuonesha kwamba Mungu haji ulimwenguni na matangazo ya hali ya juu, hajidhihirishi kwa kelele, bali anaanza safari yake kwa unyenyekevu. Na ni nani mashahidi wa kwanza wa tukio hili? Ni baadhi ya wachungaji: wanaume wenye elimu kidogo, wenye harufu kutokana na kuwasiliana mara kwa mara na wanyama, wanaoishi kando ya jamii. Hata hivyo wanafanya kazi ya kukiri ambayo kwayo Mungu mwenyewe anajitambulisha kwa watu wake (rej. Mwa 48:15; 49:24; Zab 23:1; 80:2; Isa 40:11).
Mungu anawachagua kuwa wapokeaji wa habari njema zaidi zilizowahi kusikiwa katika historia: “Msiogope; tazama, ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote: Hii itakuwa ishara kwenu: mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto na amelala horini” (Lk 2:10-12). Mahali pa kwenda kukutana na Masiha ni horini. Inatokea kwa hakika kwamba, baada ya kungoja sana, “hakuna nafasi kwa Mwokozi wa ulimwengu, ambaye kwa ajili yake vitu vyote viliumbwa (rej. Kol 1:16)” (Benedikito XVI, Utoto wa Yesu, 2012, 80). Kwa hiyo wachungaji walijifunza kwamba katika mahali pa hali ya chini sana, palipotengwa kwa ajili ya wanyama, Masiha aliyengojewa kwa muda mrefu alizaliwa na anazaliwa kwa ajili yao, ili awe Mwokozi wao, Mchungaji wao. Ni kipande cha habari kinachofungua mioyo yao kushangaa, kusifu na kutangaza kwa furaha. “Tofauti na watu wengi wanaoshughulika kufanya mambo elfu, wachungaji wanakuwa mashuhuda wa kwanza wa mambo muhimu, yaani, wokovu unaotolewa. Ni wanyenyekevu na maskini zaidi wanaojua jinsi ya kukaribisha tukio la Umwilisho” ( Barua ya Kitume Admirabile signum, 5).
Katekesi ya Baba Mtakatifu inahitimsha ikisema kuwa “Kaka na dada, tuombe neema ya kuwa kama wachungaji, wenye uwezo wa kustaajabu na kusifu mbele za Mungu, na wenye uwezo wa kulinda kile alichotukabidhi: talanta zetu, karama zetu, wito wetu na watu anaowaweka kando yetu. Tumwombe Bwana tweze kutambua katika udhaifu nguvu isiyo ya kawaida ya Mtoto wa Mungu, anayekuja kufanya upya ulimwengu na kubadilisha maisha yetu kwa mpango wake uliojaa matumaini kwa wanadamu wote.”