Papa atoa wito kuombea amani duniani:tufanye toba kwa ajili ya amani
Na Angella Rwezaula – Vatican.
Baba Mtakatifu Francisko, Jumatato tarehe 12 Februari 2025 mara baada ya Katekesi yake, kwa waamini na mahujaji waliounganika katika Ukumbi wa Paulo VI, Mjini Vatican ambayo ni Mzunguko kuhusu Jubilei ya 2025 inayoongozwa na mada ya “Yesu Kristo Tumaii letu: Utoto wa Yesu”, kama kawaidia yake hakusahau migogoro duniani.
Papa alifikri nchini nyingi zilizo kwenye vita. “Kaka na dada, tusali kwa ajili ya amani. “Tufanye kila tuwezalo kwa ajili ya amani. Tusisahau kwamba vita ni kushindwa. Daima. Hatukuzaliwa ili kuua, bali kuwafanya watu wakue. Njia za amani zipatikane.
Papa alikazai kusema “ Tafadhali, katika maombi yenu ya kila siku, ombeni amani. Ukraine iliyoteswa… jinsi inavyoteseka. Kisha, fikiria Palestina, Israel, Myanmar, Kivu Kaskazini, Sudan Kusini. Nchi nyingi sana ziko kwenye vita. Tafadhali, tuombe amani. Tufanye toba kwa ajili ya amani.”