Papa aridhia kutangazwa Wenyeheri wapya na Watakatifu wapya
Na Angella Rwezula – Vatican.
Mnamo tarehe 24 Februari 2025, wakati wa Mkutano wa Kardinali Pietro Parolin, Katibu wa Vatican, akisindikizana na Askofu Mkuu Edgar Peña Parra, Katibu msaidizi wa Masuala ya Jumla ya Sekretaieti, na Baba Mtakatifu Francisko aliridhia Baraza la Kipapa la Kuwatangaza Watakatifu na wenyeheri kutangaza amri kuhusu waamini wafuatao:
Sadaka ya maisha ya Mtumishi wa Mungu Emilio Giuseppe Kapaun, Padre wa jimbo, aliyezaliwa tarehe 20 Aprili 1916 huko Pilsen (Kansas, Marekani) na kifo chake tarehe 23 Mei 1951 katika kambi ya gereza ya Pyokton (Korea Kaskazini);
Sadaka ya maisha ya Mtumishi wa Mungu Salvo D’Acquisto, mlei mwaminifu, aliyezaliwa Napoli tarehe 15 Oktoba 1920 na kufa huko Palidoro (Italia) tarehe 23 Septemba 1943;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Miguel Maura Montaner, Padre wa jimbo na mwanzilishi wa Shirika la Ndugu wa Ibada ya Ekaristi, aliyezaliwa Palma ya Mallorca (Hispania), tarehe 6 Septemba 1843 na kufariki hapo tarehe 19 Septemba 1915;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Didaco Bessi, Padre wa jimbo, mwanzilishi wa Shirika la Masista wa Dominikani wa Mtakatifu Maria wa Rosari, aliyezaliwa tarehe 5 Februari 1856 huko Iolo (Italia) na kufariki tarehe 25 Mei 1919;
Fadhila za kishujaa za Mtumishi wa Mungu Cunegonda Siwiec, Mwamini mlei, aliyezaliwa tarehe 28 Mei 1876 huko Stryszawa - Siwcówka (Poland) na kufariki tarehe 27 Juni 1955.
Kadhalika Baba Mtakatifu pia aliidhinisha kura zilizoidhinishwa za Kikao cha Kawaida cha Mababa Makardinali na Maaskofu wa Kanisa kwa ajili ya kumtangaza Mwenyeheri José Gregorio Hernández Cisneros kuwa Mtakatifu. Alizaliwa Isnotu (Venezuela) tarehe 26 Oktoba 1864 na kufariki Caracas (Venezuela)tarehe 29 Juni 1919.
Na Mwenyeheri Bartolo Longo, waamini Mlei , azaliwa wa Latiano (Italia) mnamo tarehe 10 Februari 1841 na kufariki Pompei (Italia) mnamo tarehe 5 Oktoba 1926, na iliamuliwa kufanya baraza la makardinali kwa ajili ya tarehe za kutangazwa.