杏MAP导航

Tafuta

Mabalozi wa Mtandao wa "Talitha Kum", wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya  Maombi dhidi ya biashara ya  haramu wa binadamu. Mabalozi wa Mtandao wa "Talitha Kum", wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya kimataifa ya Maombi dhidi ya biashara ya haramu wa binadamu.  (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Papa apongeza mabalozi wahamasishaji wa Siku ya XI ya Sala na tafakari dhidi ya Biashara haramu ya Binadamu

Tuombe pamoja sala kwa maombezi ya Mtakatifu Bakhita dhidi ya Biashara haramu ya binadamu:Mtakatifu Josephine Bakhita,uliuzwa utumwani ukiwa mtoto na kuvumilia shida na mateso yasiyoelezeka.Mara baada ya kukombolewa kutoka katika utumwa wako wa kimwili,ulipata ukombozi wa kweli katika kukutana kwako na Kristo na Kanisa lake.

Na Angella Rwezaula – Vatican.

Ilikuwa tarehe 8 Februari 2015 mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, ambapo Papa Francisko akiwageukia waamini na mahujaji waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro mjini Vatican, Baba Mtakatifu alisema “Kaka na dada wapendwa, Leo, tarehe 8 Februari, ni Sikukuu ya Mtakatifu Josephine Bakhita, mtawa wa Sudan, ambaye alipokuwa mtoto alipata uzoefu wa kutisha wa kuwa mwathirika wa biashara haramu ya binadamu. Umoja wa Mama wakuu wa Mashirika ya kitawa wameandaa Siku ya Sala na Uhamasishaji dhidi ya Biashara haramu wa Binadamu. Ninawatia moyo wale wanaofanya kazi kusaidia wanaume, wanawake na watoto wanaotumikishwa, kunyonywa, kunyanyaswa kama vyombo vya kazi au starehe, ambao mara nyingi huteswa na kukatwa viungo. Ni matumaini yangu kuwa viongozi wa serikali wanaweza kufanya kazi kwa dhati kuondoa visababishi vya janga hili la aibu, ni janga lisilostahili katika jamii. Kila mmoja wetu ajisikie anajitolea kuwa sauti ya kaka  na dada zetu, ambao wamedhalilishwa katika hadhi yao. Sote sote tuwe sauti yao.”

Mabalozi wa Talitha Kum
Mabalozi wa Talitha Kum   (VATICAN MEDIA Divisione Foto)

Tarehe 7 Februari, vijana ambao ni mabalozi na walezi wao wa Mtandao wa Talitha Kum wamekutana mjini Vatican na Baba Mtakatifu Francisko. Papa Francisko anatambua jinsi mtandao huo wa Talitha Kum walivyo kundi la kimataifa, na baadhi yao wamefika kutoka mbali sana kwa ajili ya Juma hili la sala na Tafakari dhidi ya biashara haramu ya binadamu. Kwa njia hiyo, anawashukuru! Kwa namna ya pekee anawapongea vijana mabalozi dhidi ya biashara haramu ambao kwa ubunifu na nguvu daima wanatafuta mitindo mipya kwa ajili ya kuhamasisha na kuelimisha. Papa anawatia moyo kila shirika katika mtandao huo, na kwa wote binafsi, ambao wanashiriki na kuendelea kuunganisha nguvu, kwa kuwaweka katikati waathriiwa na wahanga, kuwasikiliza historia zao, kwa kutunza majeraha yao na kuongeza sauti zao. Hiyo ina maana ya kuwa mabalozi wa matumaini; na ni matumaini ya Papa kuwa Jubilei hii, watu wengine wengi wanataweza kufuata mfano wao.

Ni katika Muktadha huo, ambapo Mtandao wa Kimataifa  wa Talitha Kum,  uliondwa na Mama Wakuu wa mashirika ya Kitawa, (USG) ambao wako mstari wa mbele kuhamasisha Kampeni hii duniani kote kupitia watawa wengi waliotawanyika duniani, ili kupambana na janga hili. Kila mwaka ifikapo tarehe 8 Februari Mama Kanisa anamkumbuka Mtakatifu Josephn Bakhita mtawa Mkanosa, ambaye kiukweli alikuwa ni  mwathirika wa utumwa. Kabla ya maadhimisho hayo, Mtandao wa Talitha Kum kwa maiaka kadhaa wamekuwa wakihamasisha kuanzia tarehe 1 Februari siku za utambuzi wa hali hii mbaya, kwa kuunganisha Mabalozi wa Matumaini  ambao ni vijana kutoka ulimwengini kote ili  kuwakilisha nchi zao mjini Roma. Hata mwaka huu wa Jubilei 2025,  tangu tarehe 1 Februari 2025 wamekuwa mjini Roma ambapo matukio mbali mbali yamefanyika katika  kufikia kilele cha siku kuu ya Mtakatifu Bakhita sambamba na Siku ya Sala na Tafakari ya  kukomesha kabisa bishara haramu ya binadamu, ambayo inawakumba mamilioni ya watoto, wasichana na wavulana, na wanawake ulimwenguni kote.

Ni katika Muktadha huo ambapo pia kuna sala ya ya kusindikiza tukio hili. Tuombe pamoja sala kwa maombezi ya Mtakatifu Bakhita dhidi ya Biashara haramu ya binadamu:

Mtakatifu Josephine Bakhita, uliuzwa utumwani ukiwa mtoto na kuvumilia shida na mateso yasiyoelezeka. Mara baada ya kukombolewa kutoka katika utumwa wako wa kimwili, ulipata ukombozi wa kweli katika kukutana kwako na Kristo na Kanisa lake. Ewe Mtakatifu Josephine Bakhita, uwasaidia wale wote walionaswa katika utumwa; Uwaombee kwa Mungu wa Huruma  ili minyororo ya utumwa wao ivunjwe. Mungu mwenyewe awakomboe wote waliotishiwa, kujeruhiwa au kuteswa vibaya na biashara na usafirishaji haramu wa binadamu. Ulete faraja kwa walionusurika na utumwa huu na uwafundishe kumtazama Yesu kama kielelezo cha tumaini na imani ili wapate uponyaji wa majeraha yao. Tunakuomba utuombee na na kuwaombea: ili tusianguke katika kutojali, na ili tufumbue macho yetu na tuweze kuona taabu na majeraha ya kaka na dada zetu wengi walionyimwa hadhi yao  na uhuru wao, na usikilize kilio chao cha kuomba msaada. Amina.

Sala ya Mtatifu Bakhita
07 Februari 2025, 17:01