Papa anasumbuliwa na bronchitis,mikutano katika Nyumba ya Mtakatifu Marta
Vatican News
Baba Mtakatifu Francisko ana ugonjwa wa Bronchitis na hivyo "ili kuendelea na shughuli yake, Ijumaa tarehe 7 na Jumamosi tarehe 8 Februari 2025, mikutano itafanyika katika nyumba ya Mtakatifu Marta," anako ishi. Hayo yalielezwa na msemaji mkuu wa Ofisi ya vyombo vya habari mjini Vatican katika mawasiliano na waandishi wa habari.
"Asubuhi ya leo pia, Baba Mtakatifu alifanya mikutano katika makazi yake ya Vatican si katika Jumba la Kitume la Vatican, kwanza aliwapokea mapadre vijana na watawa wa Makanisa ya Mashariki ya kujitegemea, wakiwa katika ziara ya mafunzo huko Roma, na kisha alikutana na madaktari wa uzazi, madaktari wa magonjwa ya wanawake na wafanyakazi wa afya kutoka jimbo la Calabria.
Jumatano hata hivyo wakati wa Katekesi yake katika Ukumbi wa Paulo VI, Padre Pierluigi Giroli, ofisa wa Sekretarieti ya Vatican ndiye aliyesoma Katekesi ya Papa na baadaye mwenyewe alitoa wito kwa “nchi zinazokumbwa na vita.” Alisema msemaji mkuu.