Papa anaanzisha Tume ya Wafadhili wa michango kwa ajili ya Vatican
Vatican News
Papa Francisko, kwa maandishi ya mkono wake yaliyotiwa saini tarehe 11 Februari 2025, alianzisha Tume ya Wafadhili wa michango ya makao makuu Vatican(Commissio de donationibus pro Sancta Sede),ambayo ni tume mpya ya kazi yake maalumu katika kuhimiza michango na kampeni maalum kati ya waamini, Mabaraza ya Maaskofu na wafadhili wengine watarajiwa, huku akisisitiza umuhimu wao kwa utume na kazi za upendo kwa Vatican, pamoja na kutafuta ufadhili kutoka kwa wafadhili wenye hiari kwa ajili ya mipango maalum iliyowasilishwa na Taasisi za Curia Roma na Gavana wa mji wa Vatican; bila ya kuathiri uhuru na uwezo maalum wa kila chombo, kwa mujibu wa sheria ya sasa.”
Tume imeundwa kwa sasa na watu 5
Tume kwa sasa inaundwa na wajumbe watano (inaweza kufikia wasiozidi sita): Monsinyo Roberto Campisi, Afisa mwenye dhamana ya kumsaidia mkuu katika utekelezaji wa majukumu yake wa Sekretarieti ya Vatican, anayeiongoza, Askofu Mkuu Flavio Pace, Katibu wa Baraza la Kipapa la Kuhamaisha Umoja wa Wakristo, Sr Alessandra Smerilli, Katibu wa Baraza la Kipapa la Kuhamasisha Maendeleo Fungamani ya Binadamu, Sr Silvana Piro, Katibu Mkuu wa Utawala wa mji wa Vatican, Giuseppe Puglisi-Alibrandi, Naibu Katibu Mkuu wa Mji wa Vatican.
Uratibu na wafadhili wengine
Katika kutekeleza majukumu yake, Tume itafanya kazi kama "chombo cha kuratibu mbinu zingine za uchangishaji fedha, ziwe za kitaasisi au la, kama vile michango kwa mujibu wa Kifungu cha Sheria 1271 au Sadaka ya Mtakatifu Petro inayoheshimu asili na madhumuni ya Taasisi za kibinafsi."
Kampeni za uhamasishaji
Tume itaamua “kila mwaka kampeni za kuongeza uhamasishaji na uchangishaji fedha zitakazozinduliwa”, kubainisha “maeneo ya uendeshaji na mbinu za utekelezaji” na kufafanua “Mipango ya yote au sehemu ya shughuli. Kwa kusudi hili, inaweza kugawa kazi maalum za uendeshaji kwa mshiriki mmoja au zaidi." Zaidi ya hayo, itatambua na kutathmini kila mwaka "mipango iliyokusudiwa kukusanya rasilimali fedha muhimu kwa utekelezaji wake". Pamoja na kuweka “vipaumbele miongoni mwa miradi na vipaumbele vya mipango itakayofanyika”, Tume, “kwa kutokuwepo kwa miradi iliyowasilishwa na Taasisi, inaweza kutoa utaratibu wa kukusanya fedha za “hifadhi” zitakazotengwa kwa madhumuni ya baadae”. Udhibiti wa utekelezaji lazima upitishwe ndani ya miezi mitatu.